TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Wednesday, September 14, 2011

WAMASAI WATOA TAMKO LA KUPINGA KUPORWA ARDHI YAO, WASEMA HAWATAAMA LOLIONDO HADI KIELEWEKEMwenyekiti wa Kijiji cha Arashi wilayani Loliondo Ndugu Kyaro Alminis akionyesha msisitizo wakati akielezea Mchakato unaofanywa na Serikali wa kutaka Kuwahamisha katika ardhi yao ili Kumpisha mwekezaji wa Kiarabu anaemiliki kampuni ya OBC kutoka Falme za Kiarabu.Mwenyekiti huyo Amesema hawatahama kwasababu hapo ndipo ardhi yao ya asili ilipo.

Makundi mbali mbali ya Wanajamii walioko Pembezoni wanashiriki Tamasha la Kumila Jinsia.Hapa anaonekana Mkalimani wa Lugha ya Ishara kwa watu wenye ulemavu wa Kusikia aikiwatafsiria watu wenye ulemavu huo.

Mkurugenzi wa Shirika la Haki Ardhi Kaka Yefred Myenzi akielezea hali halisi ya Uporaji wa Ardhi unaofanywa katika maeneo Mbali mbali kwa kisingizio cha Uwekezaji.Aliyasema hayo katika Tamasha la Kumi la Jinsia linalofanyika katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP)
BADIMkurugenzi wa Mtandao Wa Jinsia Tanzania Ussu Malya Akiwaongoza Wanawake wa Kimasai Kucheza Ngoma ya Kabila la Kimasai wakati wa Kuwasilisha madai yao kutokana na Vitendo vya Uporajiwa ardhi yao Vinavofanywa na Mwekezaji wa Kiarabu anaemiliki Kampuni ya OBC

Wanaharakati kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Ruvuma wakichangia hoja ya kupinga kuporwa Ardhi ya Watanzania na Kupewa Wageni kwa Kisingizio cha Uwekezaji.Waliyasema hayo katika Tamasha la Kumi la Jinsia linaloendelea katika Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania Mabibo Dar - es - Salaam.

No comments: