TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Saturday, June 18, 2011

Katibu Mkuu CCM akiri Serikali ilikosea

KATIBU Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, amesema Serikali ilikosea kutowapeleka katika mazoezi ya vitendo wanafunzi wa vyuo vikuu, kwa kuwa hiyo ni haki yao ya msingi.

Mukama aliwaomba radhi wanafunzi hao kwa upungufu huo na kuwataka waipe Serikali mwaka mmoja ili ibadili mfumo unaotumika sasa.
Mukama alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwenye sherehe ya Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo vikuu ambao ni wanachama wa CCM walioko mjini Dodoma.

“Nawaomba radhi sana kwa kutokuwapeleka katika mazoezi ya elimu ya vitendo, lakini nawaahidi kuwa kazi hiyo tutaimaliza na haitajirudia mwakani, hivyo kuweni na amani sasa,’’alisema Mukama.

Alisema kuwa suala la kulilia elimu kwa vitendo walilokuwa wakilitafuta wanavyuo hao ni haki yao ya msingi.
Kuhusu suala la ajira kwa vijana wanaomaliza masomo, Mukama alisema katika ofisi na maeneo mengi wasomi wamekuwa wakiogopwa na baadhi ya viongozi wa sehemu hizo kwa hofu ya kunyang’anywa nafasi zao.

Mkama alikiri kuwa wasomi wengi hawatumiki ipasavyo katika jamii, ikiwamo ndani ya CCM na serikalini kutokana na hofu ya walioko madarakani kupoteza nafasi zao.

Alisema katika maeneo mengi kuna ukiritimba unaotokana na woga na hofu ya baadhi ya viongozi kwa wasomi kuwa wakiapa ajira vibarua vyao vitaota majani.
“Katika jambo kama hilo lazima tuwe makini kwani walioko ofisini wanakuwa na woga kutokana na elimu yenu kuwa wanaweza kupoteza ajira.

Akizungumzia kampeni ya Kujivua Gamba ndani ya CCM, Mukama alisema ipo na halikwepeki baada ya kugundulika kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho tawala wamekuwa wakitumia nafasi zao kwa masilahi yao binafsi.
Mukama alisema; “hakuna jambo litakalopingwa juu ya mageuzi ndani ya chama. Nakawataka mtumie (wasomi wa vyuo vikuu) elimu yenu kufanya mageuzi wanakokwenda baada ya kuhimu.

Katika sherehe hizo, Mukama aliwafahamisha wanafunzi hao kuwa katika ya vyuo vikuu vilivyopo mjini Dodoma kuna jumla ya wanafunzi 9,200 ambao baadhi yao wanahitimu katika kipindi kifupi na watakwenda kulitumikia taifa na chama

No comments: