AZMA ya Serikali kurejesha mtihani wa Kidato cha Pili itawezesha wasichana na wavulana wengi kupata elimu ya sekondari iwapo tu serikali, walimu, wanafunzi, wazazi na jamii kwa ujumla watatekeleza wajibu wao katika kufanikisha lengo hilo jema kwa taifa.
Changamoto hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurungezi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini (TAMWA), Ananilea Nkya katika ushauri wao baada ya Serikali kutangaza kurejesha mtihani wa kidato cha pili.
Nkya amesema ili mtihani wa Kidato cha Pili uongezkali inapaswa kuhakikisha inaimarisha shule za msingi za umma, ikiwemo kuwa na walimu wa kutosha kama hatua muhimu ya kuepusha be thamani kwenye elimu nchini, serikali inapaswa kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuajiri na kuwalipa mishahara inayoridhisha walimu wa shule za sekondari hasa zile za kata ambazo nyingi zimeripotiwa kuwa na uhaba wa walimu.
Katika taarifa hiyo, TAMWA imesema Seriaadhi ya wanafunzi kuingia sekondari huku wakiwa hawajui kusoma wala kuandika.
“Mwanafunzi ambaye katika shule ya msingi hakupata elimu na kujengewa tabia ya kujituma akiingia shule ya sekondari isiyo na walimu hata kama akae shuleni miaka mingapi anaweza asifaulu mitihani,” alisema Nkya katika taarifa hiyo.
Kufuatia wanafunzi wa Kidato cha Nne mwaka jana kufeli vibaya wengi wao wakiwa ni wale wa shule za sekondari za kata, serikali imetangaza kuwa mwanafunzi wa Kidato cha Pili atakayefeli mtihani wa taifa atapewa fursa ya kukariri darasa hilo mwaka mmoja lakini akifeli tena atakuwa amepoteza fursa ya kuendelea na elimu ya sekondari.
“Sisi TAMWA tunaipongeza serikali kwa kurejesha mtihani huo na tunaishauri ijitahidi kutimiza kwa vitendo wajibu wake wa kuhakikisha kuwa shule zote za msingi na sekondari zinapata walimu wa kutosha na wanalipwa vizuri ili waifanye kazi yao kikamilifu.”
Vilevile serikali ishirikiane kikamilifu na walimu, wazazi, taasisi na jamii kwa ujumla kuhakikisha kuwa shule zinakuwa na mazingira mazuri na ya usalama vinginevyo wanafunzi wengi hasa wa kike wataendelea kufeli. Mazingira hayo ni pamoja na wanafunzi kupata chakula na mabweni kwa wale wanaohitaji.
Aidha aliongeza kuwa TAMWA inatoa rai hii kutokana na ukweli kuwa wasichana wanaosoma shule za kutwa ndio wanaoathirika zaidi katika kufeli mitihani kutokana na wengi wao kukosa muda wa kujisomea nyumbani ambako wanashiriki shughuli nyingi za familia ikiwa ni pamoja na kuchota maji, kuokota kuni, kupika, usafi na kutumza wagonjwa wakiwepo wa UKIMWI.
Kadhalika walimu, wazazi/walezi na jamii nzima tunapaswa kutimiza wajibu katika kuwashauri wanafunzi kuwa na bidii na nidhamu kubwa kwenye masomo ili isitokee mwanafunzi kufeli kwa kwa sababu zinazoweza kuzuilika.
Utatiti uliofanywa na wanahabari na kuratibiwa na TAMWA katika mikoa zaidi ya 15 nchini mwaka 2010 ulionesha kuwa wanafunzi wengi katika shule za sekondari za Kata wanafeli mitihani kutokana na shule hizo kukosa walimu, chakula, mabweni kwa wale wanaohitaji na hivyo kukosa usimamizi wa walimu au wazazi.
Utafiti huo ulishuhudia baadhi ya wanafunzi wa kike wakiwa wanapangisha vyumba mitaani na wengine wakiwa wanawekwa kinyumba na wanaume wakiwepo walimu wao.
Aidha taarifa za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaonesha kuwa katika kipindi cha miaka mitano, 2004-2008, jumla ya wanafunzi 28, 590 wakiwepo 11,599 wa sekondari na 16,991 wa shule za msingi, walikatisha masomo kwa kupewa ujauzito.
Sheria ya kudhibiti makosa ya kujamiiana ya mwaka 1998 inatamka wazi kuwa kufanya mapenzi na mtoto wa kike chini ya miaka 18 ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 30 jela.
No comments:
Post a Comment