Baadhi ya Washiriki wa kongamano la kupinga mauaji ya Daudi Mwangosi na kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi wakifatilia Mjadala katika Kongamano hilo |
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Bi. Ussu Mallya akiwaongoza washiriki wa Kongamano la Kulaani mauaji ya Daudi Mwangosi na Kufungiwa kwa gazeti la Mwana Halisi kumuombea Marehemu Daudi mwangosi. Kongamano hili limefanyika katika viwanja vya Mabadiliko vilivyopo katika ofisi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar - es - Salaam Dr. Ayoub Rioba akielezea umuhimu wa kulindwa kwa waandishi wa habari wakati wakitekeleza wajibu wao.
Mmoja wa wanajopo wa Kongamano la kupinga Mauaji ya Daudi Mwangosi na kufungiwa kwa gazeti la MwanaHalisi
Mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Ndg Harold Sungusia akielezea masuala ya haki za binaadamu na hali halisi ya mauaji yanayotokea hivi sasa nchini |
Baadhi ya washiriki wa semina za Jinsia na Maendeleo GDSS wakionyesha mabango yaliokua na jumbe mbali mbali wakati wa kongamano la kupinga mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi na kufungiwa gazeti la Mwana Halisi
Katibu Mkuu wa jukwaa la Wahariri Ndg, Nevile Meena akionyesha msisitizo wakati akielezea hali halisi ya waandishi wa habari Nchini
No comments:
Post a Comment