TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Monday, May 14, 2012

Alice Foundation yapokea msaada wa chakula

mwenyekiti wa Alice Foundation akipokea chakula kutoka kwa Mch. Mkenda na wazee wa baraza kanisa la Redeemed. Kanisa la Redeemded Gospel Church tawi la Tanzania limeikabdihi Tassisi ya Alice Foundation msaada wa vyakula kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye mahitaji mbalimbali na wale wasiojiweza wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi. Akikabidhi msaada huo leo Mchungaji wa kanisa hilo lililopo Ubungo NHC mchungaji Damasus Mkenda alisema kuwa kanisa kupitia wachungaji wake mbalimbali limeona kuwa kuna hitaji kubwa lakuisaiida jamii ya watu wenye shida mbalimbali katika kata ya Ubungo ambao wanahitaji chakula. Alisema kuwa kanisa limeamua kupitia Alice Foundation kutoa msaada huo kwa kuwa taasisi hiyo imekuwa ikisaidia masuala mbalimbali ya kijamii katika kata ya Ubungo. Msaada uliokabidhiwa ni pamoja na mchele, Unga, Sukari, Maharage, Unga wa sembe, majani ya Chai ambapo alisisitiza ili kuwa na jamii iliyobora inatakiwa watu wenye uwezo kuwasaidia wale wasiokuwa nao. "Sisi hili kanisa letu lina kila sababu ya kuwasaidia watu wanaotuzunguka katika vitu mbalimbali kama vile vyakula na mengineo muhimu, hivyo kwa sasa tumeanza na hili la vyakula lakini kadiri muda unavyoenda tutawasaidia tena kwa vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu yetu ya mchango kwa jamii"alisema Mchungaji Mkenda Naye Mwenyekiti wa Alice Foundation, Alice James Dosi alisema kuwa taaisi hiyo imekuwa ikijishugulisha na masuala mbalimbali katika jamii ikiwa pamoja na kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu na hatarishi ,kuwezesha akina mama na masuala ya mazingira na masuala yanayohusu MKUKUTA Alisema kuwa katika kata ya Ubungo kuna idadi kubwa ya watoto na watu wazima wenye mahitaji maalum ambapo aliwataka watu wengine wajitokeze kusaidia masuala mbalimbali ya kuwaendeleza watu hao.. Alisema kuwa kwa wale wenye kuihitaji kutoa msaada kwa watoto hao na watu wenye mahitaji maalum kuwa wanaweza kupiga simu namba 0713 022 558 au 0756 344 9 24 au wapige 0686 179111 au wafike katika ofisi za Alice Foundation zilizopo Ubungo (NHC)

No comments: