TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Friday, November 18, 2011

TGNP YAENDESHA UTAFITI VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA NCHINI


Mwakilishi wa TGNP ndugu Badi Darus akitoa maelekezo kwa washiriki waliohudhuria warsha yaUtafiti pamoja juu ya mchango wa wanahabari katika harakati za kumkomboa mwanamke kimapinduzi na uendelezaji wa vituo vya taarifa na maarifa kwa wanawake wa mkoa wa Ruvuma, Warsha hii inafanyika katika ukumbi wa Songea Rural Sacccos katika Manispaa ya Songea.

Washiriki wa Majadiliano ya Utafiti wa uanzishwaji na uendelezwaji wa Vituo vya Taarifa na Maarifa wakijadili fursa na changamoto zinazowakabili katika harakati za ukombozi wa Mwanamke Mkoani Ruvuma.Changamoto hizo zita tatuliwa endapo kutaanzishwa vituo vya Taarifa na Maarifa kwa wanaharakati wa Mkoa wa Huo.Utafiti huu umeandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP)
Washiriki wa majadiliano ya pamoja juu ya kazi za TGNP katika Harakati za Ukombozi wa Mwanamke wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza majadiliano hayo yaliyofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa SACCOS ya Walimu Songea Vijijini .

Mwakilishi wawalemavu mkoani Ruvuma CHAVITA Asha Abdala akieleza jinsi ya kuunda mtandao wa vituo vya Habari kwa wanaharakati wa Manispaa ya Songea na Mkoa wa Ruvuma.
Moja ya mbinu zilizotumika katika kupata takwimu katika utafiti huo wa Vituo vya Taarifa na Maarifa ni kazi za Vikundi.Hapa Wanaonekana dada Judith Lugoye juu kutoka Ruvuma Press Clu na dada Janeth Fussi chini kutoka taasisi ya Restless Development wakiwasilisha moja kazi hizo za Vikundi.

No comments: