TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Thursday, October 27, 2011

ZITTO KABWE ANA HALI MBAYA.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akiwa amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Muhimbili. Kushoto ni rafiki wa yanke , Alex Kitumo.


HALI ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye alilazwa katika Hospitali ya Aga Khan, ilibadilika ghafla jana jioni kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.Zitto alilazwa Aga Khan juzi jioni baada ya kusumbuliwa na maumivu ya kichwa kabla ya kuruhusiwa na kisha kurudishwa baada ya maumivu hayo kuendelea.

Kaka wa mbunge huyo, Salum Mohamed alisema jana jioni kwamba hali ya mdogo wake ilikuwa ikiendelea vyema lakini ilibadilika ghafla na kuanza kutetemeka.

“Hali yake ya Zitto imegeuka kuwa mbaya, anatetemeka mwili mzima na sasa tunampeleka Muhimbili kwa uangalizi zaidi,” alisema Mohamed.

Jana jioni, mwandishi wa gazeti hili alimtembelea Zitto Aga Khan jana majira ya saa kumi jioni na kumkuta akiwa anaendelea vyema. Zitto, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), alisema maeneo mengine katika mwili wake yalikuwa yamepona isipokuwa maumivu ya kichwa.

Awali, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema, Erasto Tumbo alisema Zitto anasumbuliwa na ugonjwa wa kipanda uso.

Aliwataka wanachama wake chama hicho, kumuombea kiongozi huyo ili apate nafuu na kushiriki kikamilifu kwenye vikao vya Bunge vinavyotarajiwa kuanza Oktoba 8, mwaka huu.

No comments: