TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Thursday, July 14, 2011

SPIKA:MWACHENI SITA ALE PENSHENI YAKE YA USPIKA


BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limesema kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, hataondolewa katika nyumba anayoishi kwa kuwa ni Spika mstaafu.

Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisema hayo Bungeni jana wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu na kuweka wazi kwamba Maspika wote wastaafu wanapewa huduna mbalimbali na Bunge ikiwemo matibabu.

“Waheshimiwa, wakati mwingine huwa mnasema kuwa naingilia mambo kinyume na utaratibu, lakini vitu vingine mnavyouliza si sahihi kwani Samuel Sitta ni Spika mstaafu kama ilivyo kwa Pius Msekwa ambao wanahudumiwa mambo mengi na ofisi ya Bunge ikiwemo matibabu hivyo unapouliza hivyo si sahihi unatakiwa kufahamu kuwa huyu ni Spika mstaafu,” alisema Spika Makinda hivyo kumfanya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutotoa majibu zaidi kuhusu swali hilo.

“Mheshimiwa Sitta hataondolewa katika nyumbe ile aliyopewa akiwa Spika kwa sababu ni Spika mstaafu na hilo ni moja ya sharti,” alisema Makinda.

Maelezo ya Spika Makinda, yametokana na swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), aliyehoji ni lini Sitta ataondolewa katika nyumba hiyo aliyopangishiwa iliyoko Masaki ambayo hulipiwa sh milioni 12 kwa mwezi.

Aidha, alisema hivi karibuni Sitta alikwenda nchini India akiwa na mkewe na msaidizi wake kwa kutumia hati ya daraja la kwanza akiwa si Spika, hivyo kuiomba serikali imwamuru kuondoka na kwenda kuishi katika nyumba za mawaziri zilizoko Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.

No comments: