TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Monday, July 25, 2011

MRADI WA KUSAIDIA KUTATUA MATATIZO YA MAJI KWA KIGOGO NA KIWALANI WASHIKA NAFASI YA NNE


Picha mbali mbali zikiwakilisha matukio tofauti ya utafiti wa Maji yaliofanywa na Wanafunzi Kutoka chuo kikuu cha Massachusetts cha nchini Marekani Peter Kyungchul Kang na Juhyun Song Kwa wakazi wa Kata za Kigogo na Kiwalani jijini Da - es - Salaam.Mradi huu wa Maji Umeshika nafasi ya Nne Duniani.


Wanafunzi Kutoka chuo kikuu cha Massachusetts cha nchini Marekani Peter Kyungchul Kang na Juhyun Song wakipata maelezo kuhusu Mradi wa Maji wa Mburahati Kwa Mroso Water Project Kutoka kwa Mmoja wa Wasiamamizi wa Mradi huo Mzee Salvatory Komba.

Wataalaam wa Maji kutoka chuo cha Massachusetts wakimsikiliza kwa makini bwana Shabani Athuman (SHUNGU)kutoka Maeneo ya Kigogo


Hapa tukifurahi pamoja na watoto wa Kiwalani

Kaka Badi Darusi akimtwisha ndoo ya maji Mtoto Fatma Said Wakati wa utafiti huo wa maji uliofanyika maeneo ya Kiwalani.

Wataalamu wa Maji kutoka chuo kikuu cha Massachussets wakipiga Picha ya pamoja na wakazi wa kiwalani

Mtaalamu wa masuala ya Maji bwana Peter Kyungchul Kang akitabasamu mara baada ya kuchukua vipimo vya maji vinavyopatikana katika Msikiti wa Dhy Nureyn Kiwalani Daresalaam.

Mtaalamu wa maji bwana Peter Kyungchul Kang akichukua maji ili kuyapima kama ni salama kwa matumizi ya binaadamu.
href="http://4.bp.blogspot.com/-jbruhSLTkVw/Ti1LVCLoFhI/AAAAAAAAAZk/_XYvSO5nROY/s1600/DSC04601.JPG">

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kiwalani Minazi mirefu akitoa maelezo ya ramani ya mtaa wake kwa wataalamu wa masuala ya maji kutoka chuo kikuu cha Massachusetts cha nchi Marekani wakati wa Utafiti wa Mradi huo wa Maji kwa ajili ya wakazi wa Kigogo na Kiwalani.

Mtaalamu wa Masuala ya Maji na mwanafunzi wa chuo cha Massachusetts cha Nchini Marekani Bwana Peter Kyungchul Kang Wakifurahi Pamoja na Kaka Badi Darusi, Salimu Mtepetallah na Dada Felister Kisangule wakati wa Utafiti wa hali halisi ya tatizo lamaji kwa maeneo ya Kigogo na Kiwalani


Wanafunzi Kutoka chuo kikuu cha Massachusetts cha nchini Marekani Peter Kyungchul Kang na Juhyun Song wakiwa pamoja na Kaka Salimu Mtepetallah Wa Taasisi ya KYWDP wakimwangalia mtoto Zaina Mohammed wakati akichota maji kwenye kisima ambacho sio salama kwa matumizi ya Binaadamu huko Kiwalani Dar - es - Salaam.

No comments: