TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Saturday, July 9, 2011

MNYIKA AZIBANA TANESCO NA DAWASCO


MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika, amezitaka Dawasco na Dawasa, kuwasimamia kikamili wakandarasi ili kukamilisha kwa haraka taratibu za kuweka miundombinu ya maji katika kata za Kimara na Saranga.

Pia amezitaka kampuni hizo mbili, kushirikina na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), katika kufunga vifaa vya umeme ili kuwezesha nishati kufika kwenye visima vya maji.


Kwa mjibu wa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari, Mnyika alisema kauli hiyo imekuja kufuatia ziara yake katika kata hizo na kubaini kuwa kazi ya kukamilisha ujenzi wa visima haijakamilika.

"Katika ziara niliyofanya katika kata hizo nilibaini kuwa ni visima vitano tu ambavyo taratibu zake za ujenzi zinaendelea hadi sasa," alisema Mnyika.

"Nahimiza Dawasco kuanza ujenzi wa visima vingine vitatu katika maeneo ya pembezoni ya Kata za Kimara na Saranga kwa kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni ili kuwaondolea kero wakazi wa maeneo hayo,"alisema.

Mbunge huyo alisema kwa nyakati tofauti amekuwa akifuatilia agizo la Rais Jakaya Kikwete kuhusu uchimbaji wa visima vinane ili kupunguza kero ya maji kwa wananchi wanaoishi katika kata hizo.

Alisema kupitia kongamano la maji katika Jimbo la Ubungo, ilibainika kuwa ahadi ya rais ilikuwa imesahauliwa na watendaji wakuu wa mamlaka zinazohusika.

Alisema kufutia hatua hiyo walikubaliana na wananchi kulifuatilia suala hilo kwa nguvu ya umma na kuhimiza wakazi wa maeneo hayo kushirikiana katika kutekeleza azima hiyo.

"Visima hivyo vilikuwa ndio suluhisho la mpito la tatizo la maji katika maeneo ya King'ong'o, Kilungule na Mavurunza wakati serikali ikiendelea kufuatilia suluhisho la kudumu,"alisema Mnyika.

No comments: