TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Tuesday, June 14, 2011

TGNP: Bajeti hii sio ya Wananchi

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeshtushwa na hotuba ya bajeti iliyosomwa bungeni na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo kutokana na ongezeko lake kutoka sh trilioni 11 mwaka jana hadi sh trilioni 13 kwa mwaka ujao wa fedha.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya alisema hayo alipokuwa akiichambua bajeti hiyo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana na kuongeza kuwa licha ya kuwepo kwa pengo la kimapato, ongezeko la madeni na utegemezi wa bajeti kwa wahisani, ripoti ya hali halisi ya uchumi inaonesha ukusanyaji wa kodi mpaka kufikia Machi mwaka huu, ulikuwa asilimia 69 ya malengo ya kukusanya sh bilioni 6,176.2.

“Hii inamaanisha kuna pengo la asilimia 31 ya mapato ambalo ni sawa na sh bilioni 1,919.9,” alisema Mkurugenzi huyo na kubainisha kuwa matumizi makubwa ya dola katika rasimu ya bajeti na uchumi inayoonyesha serikali inachangia kudumaza thamani ya shilingi.

“Wakati huo huo ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeonesha kuwa bajeti ya Serikali ni tegemezi kwa kiasi kikubwa kwa wahisani na deni la taifa linakua kutoka sh trilioni 7.6 mwaka juzi hadi sh trilioni 10.5 mwaka jana ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 38 ya pato la taifa,” alisema.

Aidha, alisema Mkulo alibainisha gharama za uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba mwaka jana, zilitumika kama zilivyopangwa, bila kutoa maelezo ya kina.

“Tunadai ufafanuzi juu ya yafuatayo. Serikali ilipanga kutumia shilingi ngapi, ilitumia shilingi ngapi, fedha za ndani zilikuwa ngapi na fedha za wahisani zilikuwa ngapi? Pia tunahoji wanawake wa Tanzania wamenufaika vipi kwa fungu hili?” alihoji Mallya.

Kwa upande wa kipaumbele cha nishati, serikali inawashauri wananchi kuanza kutumia vyanzo mbadala vya umeme wa jua, upepo na nishati inayotokana na biogesi na kutumia kwa uangalifu umeme uliopo.

No comments: