TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Tuesday, June 21, 2011

KANUMBA AWA BALOZI WA HESHIMA WA MPANGO WA MAPINDUZI YA KILIMO NCHINI


Kaka Badi Darusi nae hakua nyuma katika kuurudi Mduara wakati wa uzinduzi huo wa ripoti ya hali halisi ya kilimo nchini uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP)Mabibo Dar- es- salaama.

Wana Kichochoro nao hawakubaki nyuma katika kuucheza mduara siku ya uzinduzi huo.Mbele anaonekana kaka Eliabu Maganga akimuongoza kaka Badi Darusi katika kuucheza mduara.

Balozi wa Heshima wa mpango wa kilimo nchini kupitia shirika la OXFAM Steven Kanumba akitoa hotuba ya shukrani mara baada ya Kufanya uzinduzi rasmi
Baadhi ya kina mama wakicheza na kufurahi pamoja na Kanumba wakati wa uzinduzi huo.

Balozi wa heshima wa mpango wa kilimo nchini Steven Kanumba akionyesha umahiri wake katika kucheza Segere hii ilikua mara baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo ya hali halisi ya kilimo nchini

Wanaharakati kutoka mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)Kutoka kushoto ni dada Anna Sangai,Anna Kikwa,Marry Nsemwa na Dada Fides Chale wakionyesha hisia zao za furaha mara baada ya Uzinduzi rasmi kufanyika.

Steven Kanumba akiiunua chapisho juu la hali halisi ya Kilimo nchini mara baada ya kulizindua.(Picha zote na Badi Darusi aka kazi bila ya kipato)

Mkurugenzi wa Oxfam akiwa na kina Kanumba na dada Lilian Liundi wakiinua machapisho ya Ripoti ya hali halisi ya kilimo Nchini mara baada ya kufanya uzinduzi rasmi.

Mkurugenzi wa OXFAM akisoma hotuba kwa mgeni Rasmi Bwana Steven Kanumba.


Steven Kanumba akiwa na wageni wengine katika meza kuu,Kushoto ni dada Lilian Liund kutoka Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP)NA Kulia ni Mkurugenzi wa shirika la OXFAM.Uzinduzi huu wa Kampeni ya Haki ya kilimo ulifanyika katika viwanja vya Ofisi ya mtandao wa Jinsia Tanzania (Tgnp)

No comments: