TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Sunday, June 19, 2011

Fabregas, Nasri wataka kubaki Arsenal


NAHODHA wa klabu ya Arsenal, Cesc Fabregas akichuana na mchezaji wa Man U


NAHODHA wa klabu ya Arsenal, Cesc Fabregas amesema anapenda kuichezea Arsenal msimu ujao ila hafahamu kama kocha Arsene Wenger wa Arsenal bado anamuhitaji.

Fabregas alisema hayo baada ya kuona habari nyingine zinazotolewa zinamuhusisha yeye kuahamia klabu ya Barcelona ya Hispania.

Zipo taarifa pia klabu za Manchester City na Real Madrid zinamuhitaji mchezaji huyo anayecheza nafasi ya kiungo na ana miaka 24.

"Mimi ninafurahi nilipo na kama nitasema kitu chochote nitakuwa nadanganya, mimi ni mchezaji wa Arsenal, tuna timu nzuri na kocha mzuri, kama nikiondoka Arsenal nitasema tena maneno hayo siku nitakapokuwa naondoka,"alisema Fabregas.

Alisema,"Bado sijazungumza na kocha wangu, yeye ndiye anayefanya maamuzi hivyo sifahamu kama ameniuza au hajaniuza, kila mtua ana njia yake kutafsiri jambo, lakini katika suala langu siyo tu mchezaji mwenye maamuzi."

"Mimi nina thamani yangu, nimeka Arsenal kwa miaka nane, nimetoka Barcelona nikiwa na miaka 16,siwezi kufanya mambo ambayo yataniharibia kila kitu, ni vizuri watu wakafahamu nipo katika wakati mgumu wa maamuzi,

Kuhusu Barcelona, kiungo Fabregas alisema,"Barca ni timu bora kabisa duniani na ukiwa unaichezea klabu ile una uhakika wa kutwaa mataji, hakuna mchezaji ambaye hapendi kushinda mataji mbalimbali, huyo atakuwa akidanganya."

Wakati huo huo; klabu ya Lille imethibitisha kwamba mipango ya mshambuliaji raia wa Ivory Coast, Gervinho kununuliwa na klabu ya Arsenal kwa pauni 12milioni inaelekea kumalizika.

Wakati huo huo wakala wa Samir Nasri naye amesisitiza kuwa mchezaji huyo anataka kuendelea na mazungumzo na uongozi wa Arsenal ili aendelee kuichezea klabu hiyo licha ya kutakiwa na klabu mbalimbali.

Nasri anakaribia kumaliza mkataba wake na hivi karibuni amekuwa akitakiwa na klabu za Inter Milan, Manchester United, Real Madrid na Juventus, lakini Nasri amekuwa akitaka mkataba mpya na Arsenal ,lakini uwe wa fedha nyingi.

Wakala wa Nasri anayeitwa Alain Migliaccio alisema,"Ninataka kutoa ufafanuzi kuhusu Nasri kusaini mkataba mpya, bado mazungumzo yanaendelea kati ya Nasri na Uongozi wa Arsenalna tunatarajia hivi karibuni tutazungumza na kocha wa Arsenal, Arsene Wenger.

No comments: