TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Friday, October 10, 2008

HII NI SIASA AU VITA TARIME


(PICHA HII KWA HISANI YA IPPMEDIA)


Wanaharakati,Hivi ni lazima chama cha Mapinduzi(CCM)kishinde kila uchaguzi?Hali ya Tarime sasa inatishia amani na kuna kila dalili ya CCM kwenda na maji,Sasa kinachotumika ni nguvu ya dola,Watu wanapigwa ovyo na hata wengine kufikia hatua ya kuuwawa.Polisi wanaokadiriwa 3000 na dhana za kivita zimeelekezwa Tarime sasa kwa faida ya nani kama sio kutumika kuibeba CCM?Wanaharakati, Tarime ina kila dalili ya kuelekea kwenye machafuko kwa kutaka kutawaliwa kwa nguvu zote.
Nahisi ni upigaji wa kura ndani ya mfumo wa kijeshi. Hii inaonyesha bila kutumia jeshi ushindi ni kitendawili.
Pia kunavitendawili vingi sana Tarime,kama majina ya wapiga kura kokosekana, msimamizi wa uchaguzi kudai atahakikisha watu wanapiga kura pamoja na kasoro zilizojitokeza kwenye majina yao, komputa kukosea????
Hivi kati ya komputa na mtumiaji wa komputa ni nani anayekosea?
Inabidi tulivalie njuga suala la tume huru ya uchaguzi kama tulivyo livalia njuga suala la EPA na kaka zake.
Imefikia hatua sasa viongozi wetu mkubali ukweli na kuicha Demokrasia ichukue mkondo wake kwa wanachi walio wengi kuchagua viongozi wanao wapenda.

NYIE WANAHARAKATI WENZANGU MWALONGAJE KUHUSU TARIME?NITUMIE MAONI YAKO SASA.......

No comments: