Msanii maarufu wa Filamu nchini Steven Kanumba akiwa na rafiki yake kipenzi wakati wa uhai wake Patcho Mwamba. Steven Kanumba alifariki jana majira ya saa tisa Usiku nyumbani kwake Sinza jijini Dar - es - Salaam mara baada ya kutokea ugomvi.Mwili wa marehemu Steven Kanumba umehifadhiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.Habari zaidi tutawaletea baadae.
Marehemu Steven Kanumba akiwa na Wapiga Picha wa Filamu ya Ndoa yangu wakati wa kupiga picha za filamu hiyo.Kanumba amefariki jana nyumbani kwake majira ya Saa tisa usiku mara baada ya kutokea ugomvi nyumbani kwake.
Marehemu Steven Kanumba akitoa maelekezo kwa waigizaji wakati wa kuchukua picha za filamu yake ya mwisho ya ndoa yangu.
Marehemu Steven Kanumba akiwa na Jacline Wolper wakati wa kurekodi filamu yake ya Mwisho ya Ndoa yangu.
Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya wasanii wenzake wa filamu Steven Kanumba amefariki dunia usiku huu wa saa 9 kutokana na kupata ajali ambayo ilimpelekea kudondoka chini na kufikia kichwa usiku huu nyumbani kwake Sinza. Taarifa zaidi zitaendelea kukujia kila tutakapozipata. Mwenyezi mungu ailaze mahala pema peponi roho ya Steven Charles Kanumba.
UPDATES: Msiba upo nyumbani kwake Sinza karibu na Vatican City - watu wengi wanakuja kutoa pole.
UPDATES: Mwanamke anayeitajwa kuhusika na tukio la kifo cha Kanumba japo bado haijathibitishwa ni Muigizaji Lulu.
UPDATES: Watu tofauti kutoka kada tofauti, wakiwemo wasanii wa filamu na muziki wanazidi kufurika nyumbani kwa Kanumba hapa Sinza, simamzi imetawala kwa kiasi kikubwa watu wanalia sana. Kiukweli inasikitikitsha.
UPDATES: Kumekua na taarifa nyingine ambazo hazijadhibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.
UPDATES: Ndugu wa marehemu wakiwemo mdogo wake amethibitisha kifo cha kaka yake na kusema taarifa rasmi ya kifo chake itatolewa asubuhi.
UPDATE:
Taarifa nilizozipata sasa hivi kutoka kwa mwigizaji Dino, ni kwamba kweli mwigizaji STEVEN KANUMBA amefariki dunia na inaaminika chanzo cha kifo chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake, alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.
Polisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba muda mfupi uliopita baada ya kuwachukua waliokua wanaishi na Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya kilichotokea.
Bado watu wanazidi kuongezeka nyumbani kwa Kanumba ambapo tayari idadi kubwa ya wasanii wenzake wamefuka pamoja na watu mbalimbali, Blog hii itaendelea kukufahamisha kinachoendelea kadri taarifa zitakavyozidi kupatikana.
Ila kumekua na taarifa nyingine ambazo hazijathibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake ambae anatajwa kuwa ni mwigizaji LULU kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.
‘Inasemekana’ Kanumba wakati akijiandaa kutoka saa sita usiku aliingia bafuni kuoga, alipotoka alimkuta Lulu akiongea na mwanaume mwingine kwenye simu ndipo alipokasirika na ugomvi kuanza.
Alipelekwa hospitali Muhimbili ambako muda mfupi baadae alifariki dunia, mwili wake bado uko katika chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili hospital.
No comments:
Post a Comment