Baadhi ya Mabasi kama yanavyoonekana katika Picha yakiwa katika foleni ya Kusubiri kuondoka kufuatia zoezi la ghafla la ukaguzi wa Leseni za Madereva lililofanywa na Polisi wa Usalama barabarani leo asubuhi.
Kamanda wa Polisi wa Usalama barabarani Bwana Mohammedi Mpinga akiwasihi baadhi ya madereva waliotishia kugoma kusafirisha abiria kufuatia kudai maslahi zaidi katika ajira zao na kupinga unyanyasaji wanaofanyiwa na jeshi la polisi wa Usalama barabarani Tanzania.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar - es - Salaam, Bwana Suleimani Kovaakiwasihi baadhi ya madereva waliotishia kugoma kusafirisha abiria kufuatia kudai maslahi zaidi katika ajira zao na kupinga unyanyasaji wanaofanyiwa na jeshi la polisi wa Usalama barabarani Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana akiwasihi baadhi ya madereva waliotishia kugoma kusafirisha abiria kufuatia kudai maslahi zaidi katika ajira zao na kupinga unyanyasaji wanaofanyiwa na jeshi la polisi wa Usalama barabarani Tanzania.
Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva waendao mikoani akielezea nia yao ya kufanya mgomo nchi nzima ili kudai maslahi zaidi na Kupinga manyanyaso wanayofanyiwa na polisi wa Usalama barabarani
Foleni ya kwenda chooni kujisaidia nayo ilikua kubwa isivyo kawaida.Hapa wanaonekana baadhi ya abiria wanaokwenda nchi na mikoa tofauti wakiwa katika foleni hiyo.
Wamama wajawazito na watoto wachanga waliteseka sana leo kwa kadhia hiyo ya ukaguzi wa Leseni uliofanywa ghafla na askari wa usalama barabarani.
No comments:
Post a Comment