Basi la abiria la Kampuni ya Upendo linalofanya Safari zake kati ya mkoa wa Iringa na Dar - es - Salam limepata ajali Mkoani Morogoro likiwa linatoka Dar - es - Salam Kuelekea mkoani Iringa.Watu wawili wamekufa papo hapo na idadi ya majeruhi bado haijajulikana. Miili ya marehemu na majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro. Habari zaidi tutawaletea kadri zitakavyokua zinatufikia.
No comments:
Post a Comment