Haya ni magari ya makombora ya masafa marefu.
Mara baada ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dk. Jakaya Kikwete kukagua vikosi vya ulinzi na usalama na vikosi hivyo kutoa heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu huyo, kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania leo katika uwanja wa Uhuru, yalifuatia maonyesho ya vifaa vya kijeshi vilivyoonyeshwa na jeshi tukufu la Tanzania JWTZ, ambapo askari wa jeshi hilo wakiwa wakakamavu, walipita na kuonyesha vifaa vya kivita kama linavyoonekana na gari hili ni la Rada hutumiwa na jeshi la wanamaji.
No comments:
Post a Comment