MBUNGE wa Jimbo la Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, ambaye Desemba 8 mwaka huu alienguliwa katika nafasi ya ukatibu mwenezi, huenda akavuliwa uanachama. Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa mbali na kuvuliwa wadhifa huo, mbunge huyo, sasa anakabiliwa na hatua nyingine ngumu zaidi kisiasa, baada ya uongozi wa chama hicho kutaka kumvua uanachama. Kwa mujibu wa habari hizo, hatua hiyo imepangwa kufikiwa Jumamasi hii, wakati Halmashauri Kuu ya chama hicho itakapoketi kwa dharura jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali ikiwamo, suala la Kafulila. Katibu mkuu wa NCCR Mageuzi Samwel Ruhuza alithibitisha jana maandalizi ya kikao hicho cha dharura lakini, akasema agenda zake hazijapangwa. "Ni kweli Halmashauri kuu imeitishwa kwa dharura Jumamosi hii jijini Dar es Salaam na baadhi ya wajumbe wameanza kufika," alisema Ruhuza na kuongeza: “Mkutano utafanyika keshokutwa (Jumamosi) lakini bado hatujapanga eneo tutakapofanyia. Tukipanga tutawajulisha waandishi wa habari,” alisema Ruhuza. Alipoulizwa iwapo moja ya ajenda za mkutano huo ni kumjadili Kafulila, katibu mkuu huyo alisema kwamba hawezi kulizungumzia suala hilo sasa hadi muda mwafaka utakapowadia. Chanzo cha habari ndani ya chama hicho kimeeleza kuwa kanuni za nidhamu na usuluhishi za NCCR ukurasa wa 49, jedwali la saba kipengele cha kwanza na cha pili, zinaonyesha kuwa Kafulila anaweza kutimuliwa uanachama na huo baada ya kuondolewa uongozi. “Kafulila alitakiwa kupingana na Mbatia (Mwenyekiti) ndani ya vikao vya chama na siyo katika vyombo vya habari na sio yeye tu, wale wote waliohusika kufanya jambo hilo nao watahusishwa”, kilisema chanzo hicho na kuongeza: “Suala hili karibu litafikia tamati na kumaliza mvutano ndani ya chama; Kafulila kavunja kanuni nyingi za chama sijui itakuwaje ngoja tusubiri uamuzi.” “Nina mpango wa kuiboresha hii idara (Uenezi) ili kuipa makali, atakapoteuliwa mtu mwingine wa kuziba nafasi hiyo vyombo vya habari vitaelezwa,” alisema Ruhuza Alipoulizwa kuhusu hatma ya Kafulila, alisema suala hilo hawezi kulizungumza bali linaweza kujadiliwa katika vikao vya ndani vya chama. Mbatia Akizungumza na Mwananchi Mbatia alisema hawezi kuzungumza masuala ya utendaji wa chama katika vyombo vya habari na kutaka atafutwe Katibu Mkuu, ili alizungumzie suala hilo. Katika hatua nyingine Ruhuza amesema hali ya siasa ndani ya chama hicho sasa ni shwari na kwamba kitaendelea kuwashughulikia wanachama wake wanaoonekana kuwa ni kikwazo kwa kutengeneza makundi yenye lengo la kukibomoa. Alisema kuenguliwa kwa Mbunge huyo ni adhabu tosha na kwamba chama hicho kitaendelea kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi. “Kama unavyo fahamu Kafulila ni Mbunge na anamajukumu mengi katika jimbo lake sasa hatuwezi kuendelea na nafasi hiyo ambayo inahitaji mtu wa kufanya katika muda wote wakazi ndio mana tumeamua kumpumzisha,” alisema Hata hivyo Katibu Mkuu huyo alisema suala la Kafulila sasa limekwisha na haipaswi tena kulizungumzia kwa sababu tayari chama kimeshatekeleza majukumu yake kwa kufuata Katiba ya chama hicho. |
TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE
Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com
Thursday, December 15, 2011
Kafulila akalia kuti kavu NCCR.Wafikiria Kumvua Ubunge
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment