Mwakilishi wa TGNP ndugu Badi Darus akitoa maelekezo kwa washiriki waliohudhuria warsha yaUtafiti pamoja juu ya mchango wa wanahabari katika harakati za kumkomboa mwanamke kimapinduzi na uendelezaji wa vituo vya taarifa na maarifa kwa wanawake wa mkoa wa Ruvuma, Warsha hii inafanyika katika ukumbi wa Songea Rural Sacccos katika Manispaa ya Songea.
Washiriki wa Majadiliano ya Utafiti wa uanzishwaji na uendelezwaji wa Vituo vya Taarifa na Maarifa wakijadili fursa na changamoto zinazowakabili katika harakati za ukombozi wa Mwanamke Mkoani Ruvuma.Changamoto hizo zita tatuliwa endapo kutaanzishwa vituo vya Taarifa na Maarifa kwa wanaharakati wa Mkoa wa Huo.Utafiti huu umeandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP)
Washiriki wa majadiliano ya pamoja juu ya kazi za TGNP katika Harakati za Ukombozi wa Mwanamke wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza majadiliano hayo yaliyofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa SACCOS ya Walimu Songea Vijijini .Mwakilishi wawalemavu mkoani Ruvuma CHAVITA Asha Abdala akieleza jinsi ya kuunda mtandao wa vituo vya Habari kwa wanaharakati wa Manispaa ya Songea na Mkoa wa Ruvuma.
No comments:
Post a Comment