Karani mwongozaji Wapiga kura kutoka kituo cha Mwamashimba Shule ya Msingi Ndugu Mhojaa Mwanamadushi akiwajibika leo Asubuhi katika kituo hicho.
Wapiga Kura wakipiga kura katika vijiji vya Igurubi na Mwagala katika jimbo la Igunga leo asubuhi
Wakazi wa Kijiji cha Ibole katika Jimbo la Igunga wakiangalia majina yao muda mfupi kabla ya Kupiga kura leo asubuhi.
Uchaguzi mdogo unaondelea hivi leo Katika Jimbola Igunga kuziba nafasi ya aliekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Ndg. Rostam Aziz umekumbwa na Kasoro kadhaa ndogo ndogo ikiwemo baadhi ya vituo kuchelewa Kufunguliwa na Baadhi ya mawakala wa Chadema kukutwa na madaftari yenye orodha na picha Wapiga.
Katika utetezi wao chama cha Chadema wamesema kuwa madaftari hayo ni haki yao na wanalinda kura zao zisichakachuliwe na CCM.
Nae msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hili ndugu Magayane T. Protace amesema tukio hilo la Mawakala wa Chadema kukutwa na madaftari hayo sio uvunjifu wa sheria na ameruhusu vyama vingine wayatumie kama wanayo ili kuangalia usahihi wa wapiga kura wao.
Tukio lingine la kusikitisha ni la kuzuiwa kuingia katika vituo vya kupigia kura kwa Waangalizi wa Uchaguzi wa ndani licha ya kwamba walikua na Vitambulisho na barua za Kuwatambulisha katika kazi yao. Tukio hili limejitokeza sana katika kata ya Igurubi katika vijiji vya Kalangale kituo cha ofisi ya Kijiji na kituo cha shule ya sekondari Igurubi katika kijiji cha Igurubi.
Mpaka kufikia zoezi la upigaji kura linaendelea kwa amani licha ya kukumbwa na upungufu wa wapiga kura katika vituo vya kupigia kura.
No comments:
Post a Comment