Viingilio vya pambano la Yanga na Simba litakalofanyika Oktoba 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom vitakuwa kama ifuatavyo;
Viti vya kijani na bluu kiingilio kitakuwa sh. 5,000, viti vya rangi ya chungwa ni sh. 7,000, VIP C sh. 10,000, VIP B ni sh. 15,000 wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.
Mwamuzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Oden Mbaga kutoka Dar es Salaam ndiye atakayechezesha mechi namba 78 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Simba itakayofanyika Oktoba 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waamuzi wasaidizi katika mechi hiyo ambao wote wanatambuliwa na FIFA ni Hamis Chang’walu wa Dar es Salaam ambaye atakuwa namba moja, na John Kanyenye (Mbeya) atakayekuwa namba mbili.
Mtathimini wa waamuzi (referee assessor) atakuwa Soud Abdi kutoka Arusha wakati kamishna wa mchezo huo ni Mohamed Nyange kutoka Dodoma.
No comments:
Post a Comment