Hapa ilikuwa ni piga nikupige.
Francis Miyeyusho akikwepa konde zito la Mbwana Matumla
Bingwa Mpya wa UBO katika uzito wa Bantum,Francis Miyeyusho akifurahia ubingwa wake huo wakati akivishwa mkanda wake na Mlezi wa Mchezo wa Ngumi hapa nchini,Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Afande Suleiman Kova huku Diwani wa Kinondoni,Mh. Abbas Tarimba akiangalia.Francis Miyeyusho kanyakuwa ubingwa huo baada ya kumchakaza vibaya Bingwa wa Zamani UBO,Mbwana Matumla katika mchezo uliomalizika jana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee hall.
Bondia Francis Miyeyusho akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mpambano kuisha na yeye kuibuka bingwa mpya wa UBO baada ya kumchapa Mbwana Matumla kwa point.
No comments:
Post a Comment