Kufuatia matokeo ya kufungwa na watani wao wa jadi 1-0 , taarifa kutoka chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya dressing room ya Simba SC ni kwamba Haruna Moshi Boban amempiga vichwa mchezaji mwenzie Mganda Emmanuel Okwi kwa madai ya kuikosesha ushindi timu kwa kukosa mabao mengi ya wazi.
“Haruna amempiga Okwi baada ya mechi kuisha huku akimtuhumu kuikosesha timu ushindi kwa kukosa kufunga katika nafasi za wazi.Baada ya kumpiga Okwi, Haruna ameondoka hapa uwanjani peke yake bila kuongozana na wachezaji wenzie,” kilisema chanzo cha habari.
Mpaka sasa haijajulikana Okwi ameumia kwa kiasi gani kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa Boban.
No comments:
Post a Comment