TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Friday, September 9, 2011

WATU 610 WAKADIRIWA KUFA MAJI KATIKA AJALI YA MELI YA MV SPICE ZANZIBAR

MELI YA LCT SPICE ISLANDERS IKIWA IMEZAMA KATIKA PWANI YA NUNGWI KAMA INAVOONEKANA KATIKA PICHA.PICHA KWA HISANI YA MOHAMED AHMED WA ZANZINET

Meli ya LCT SPICE ISLANDERS imebinuka na kuzama katika Bahari ya Hindi huko ktika Pwani ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ikielekea Kisiwani Pemba huku ikiwa imebeba abiria 610 na shehena ya mizigo.
Habari kutoka sehemu ya tukio ni kwamba watu 250 wameokolewa na boti nyengine ya sea express kati ya hao 610, maiti hadi sasa ni 14 na bado juhudi zinaendelea na afya zao ni mbaya kutokana kunywa maji mengi.

Taarifa ya kuzama kwa meli hiyo zimetolewa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundo Mbinu wa Serikali wa Mapinduzi Zanzibar Mh. Issa Haji Ussi mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa Nahodha wa meli ya Mv Jitihada inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliokuwa inafanya safari zake kutoka Unguja kwenda katika Bandari ya Mkoani kisiwani Pemba.

Jitihada za kuwaokoa waliozama bado zinaendelea kwa kuwahusisha wadau mbali mbali wa vyombo vya majini na jeshi la Polisi lililotowa helkopta yake kwa ajili ya Uokoaji.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kutoa taarifa zaidi kadri zoezi la uokoaji linavyoendelea na kuwataka Wananchi kuwa Watulivu.

BLOG HII ITAENDELEA KUWAHABARISHA KADRI TAARIFA ZAIDI ZITAKAVYOKUWA ZINATUFIKIA.

No comments: