TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Thursday, January 17, 2013

Presicion Air yazindua safari za Mbeya


Kaka Badi Darusi akipanda katika ndege no PW 401 ilionza safari zake kati ya Da - Mwanza na Mbeya

Kaka Allan Mihayo akiwa katika uwanja wa Ndege wa Songwa Mjini Mbeya tayari kwa safari ya kuelekea Dar

Kaka Darusi ndani ya Precion

Baadhi ya Abiria waliokua kwenye ndege no PW 401 wakiwa katika bara bara ya kukimbilia ndege katika Uwanja wa Julius Nyerere International Airport

Wakazi wa Mbeya  na Mikoa ya nyanda za juu Kusini jana walifuraia ujio wa ndege ya Precision iliyoanza safari zake kati ya Dar-Mwanza- Mbeya siku ya leo wakieleza kuwa ukombozi wa kiuchumi wa mikoa hiyo umewadia.

Hafla ya kupokea ndege hiyo ilihudhuliwa na umati mkubwa wa wakazi wa mkoani Mbeya waliofurika katika uwanja huo wa kimataifa wa Songwe huku Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Norman Sigala akiwaeleza wananchi kuwa wanatakiwa wautumia usafiri huo kujenga uchumi wa mkoa huo.

Ndege hiyo imewasili leo majira haya ya asubuhi maalumu kabisa kuzindua safari zake kufuatia kukamilika kwa uwanja huo wa kimataifa unaoweza kupokea ndege kubwa na ndogo.

Wadau wa usafiri wa anga mkoani humo wamefurahishwa na ujio wa ndege hiyo wakieleza kuwa utakuza na kuchochea uchumi wa Mkoa huo, pia walitoa wito kwa kampuni nyingine kujitokeza kuanzisha safari zao kwani wahitaji wa wasafiri ni wengi.

No comments: