VIONGOZI wa dini za Kikristo na Kiislamu wamejitosa katika sakata la Dk Steven Ulimboka ambaye yuko nchini Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kutekwa na kupigwa na watu wasiojulikana pamoja na mgomo wa madaktari kwa kufanya mkutano na viongozi wa Jumuiya ya madaktari na wanaharakati jijini Dar es Salaam jana.
Viongozi
hao walipendekeza iundwe kamati huru ya kuchunguza tukio la kupigwa Dk
Ulimboka mapema iwezekanavyo ili kupata ukweli wa kilichotokea.
Pia
viongozi hao walishauri kuwa Rais Kikwete akutane na madaktari pamoja
na viongozi wa dini ili kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wao unaoendelea
nchini hivi sasa.Viongozi hao pia wameitaka Serikali kutoa ulinzi kwa
Dk Ulimboka na madaktari wote wengine ili kuwahakikishia usalama wa
maisha yao.
Akisoma
tamko la viongozi hao, Mkurugenzi wa Baraza la Habari la
Kiislamu(Bahakita), Hussein Msopa kwa niaba ya viongozi hao alisema
kwamba, kuundwa kwa kamati huru ya uchunguzi itasaidia kupata ukweli
wa tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dk Ulimboka na kuwezesha kubaini
wahusika wa tukio hilo.
“Tukio la kutekwa, kuteswa na kutupwa katika Msitu wa Pande Dk Ulimboka ni la kusikitisha… na tunamuomba Rais Kikwete aunde tume huru itakayojumuisha madaktari wenyewe, viongozi wa dini, wanaharakati na wanasheria kubaini kiini cha tatizo hilo.” alisema Msopa.
“Tukio la kutekwa, kuteswa na kutupwa katika Msitu wa Pande Dk Ulimboka ni la kusikitisha… na tunamuomba Rais Kikwete aunde tume huru itakayojumuisha madaktari wenyewe, viongozi wa dini, wanaharakati na wanasheria kubaini kiini cha tatizo hilo.” alisema Msopa.
Kauli
ya viongozi hao wa dini ni ya kwanza kutolewa kwa pamoja tangu kutokea
kwa tukio la kutekwa, kupigwa na kutupwa kwa Dk Ulimboka katika Msitu
wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Viongozi
hao pamoja na kudai tume huru pia waliomba Serikali kufuta kesi
iliyofungua dhidi ya madaktari waliofukuzwa kutokana na mgomo na
kuwarejesha kazini ili kumaliza mgomo huo waliodai unaathiri afya za
Watanzania.
Tamko
hilo limekuja siku chache tangu Serikali ilipofungua kesi dhidi ya
madaktari waliogoma kwa Baraza la Madaktari Tanzania ikilitaka kufanya
uchunguzi na kuchukua hatua stahiki kwa madaktari hao.
Msopa alitaja sababu ya viongozi hao kuungana na wanaharakati kutafuta suluhisho la mgomo huo kuwa ni kuona Watanzania wanazidi kuteseka kwa kukosa huduma za matibabu.
Msopa alitaja sababu ya viongozi hao kuungana na wanaharakati kutafuta suluhisho la mgomo huo kuwa ni kuona Watanzania wanazidi kuteseka kwa kukosa huduma za matibabu.
“Tunafahamu
kwamba, Rais Kikwete ameweza kutatua migogoro mingi mfano mgogoro wa
Chadema, suala la Katiba Mpya, migogoro ya Zanzibar, hivyo pia sasa
tunaamini katika hili la madaktari ataweza kulitafutia ufumbuzi,”
alisema Msopa.
Kwa
upande wake Mchungaji Lawrance Mzava wa Kanisa la Kiinjili la
Assemblies of God (EAGT) Ubungo ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kamati
hiyo, alisema hiyo itakuwa njia sahihi ya kumaliza mgogoro huo
unaotikisa nchi kwa sasa.“Njia sahihi ya kuondoa mgogoro huo ni kufanya mazungumzo ambayo yatasaidia kufikia makubaliano yatakayoleta ufumbuzi wa kudumu wa mgomo wa madaktari,” alisema Mzava na kuongeza:
“Sisi tunaamini kuwa njia sahihi ya kuleta suluhu ya mgogoro huu ni kwa Rais Kikwete kukutana na kufanya mazungumzo na sisi (viongozi wa dini) na madaktari,” alisema.
Mgomo
Mgomo wa madaktari unaoelezwa kumalizika kwa kusuasua ulianza Juni 23 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI) na kusambaa hospitali mbalimbali nchini, madaktari wakitoa madai mbalimbali kuitaka Serikali iyatekeleze.
Hata hivyo, hadi jana upatikanaji wa huduma MNH na Taasisi ya Mifupa (MOI), umezidi kuzorota, huku baadhi ya madaktari wakisema tukio la Dk Ulimboka limewapunguzia ari ya kufanya kazi.
Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina, baadhi ya madaktari wa MNH, walisema tukio la kutekwa, kupigwa na kutupwa kwa Dk Ulimboka limewatisha.
“Kwa sasa madaktari hawana ari, hata wakifika eneo la kazi bado suala la kufanya kazi ni kitu kingine, lakini kitendo cha kutekwa kwa Dk Ulimboka kimetutisha sana, ” alisema mmoja wa madaktari hao wa MNH.
Uchunguzi wa Blog hii umebaini kuwapo kwa baadhi ya madaktari bingwa katika MNH pamoja na MOI, ambao nao walithibitisha kuwa utendaji kazi hauwezi kuwa wa ufanisi kwa njia ya kulazimishwa.
“Serikali inachotakiwa siyo kulazimisha, inapaswa kusikiliza na kutatua hoja, sisi madai yetu yamepotoshwa, hatuna vifaa vya kufanyia kazi, lakini wananchi hilo hawalielewi,” alisema mmoja wa madaktari hao.
Hata hivyo, Msemaji wa MNH, Eminael Aligaesha alisisitiza kuwa huduma katika hospitali hiyo zinarejea hatua kwa hatua.
No comments:
Post a Comment