Umati wa Watu waliojitokeza katika Mazishi ya Marehemu Omary Maunda aliefariki kwa Ugonjwa wa kupungukiwa damu mara kwa mara Mwilini.Omary Maunda ambae alikua mwanafunzi wa zamani wa Ununio Boys Islamic High School (2001 -hadi 2003.Mpaka anakufa Marehemu Omary Maunda alikua mtumishi wa Jeshi la Magereza mwenye cheo cha Afisa mkaguzi Msaidizi(Assistant Inspector.Ameacha mke na mtoto mmoja
Kaburi alilohifadhiwa Marehemu Omary Maunda kama linavyoonekana
Baadhi ya Wanafunzi wa zamani wa Ununio Boys High school bwana Seif Mikoi alievaa tshirt nyekundu na Abdulatif Said mwenye shati jeupe wakishiriki kikamilifu katika mazishi ya mwanafunzi mwenzao wa zamani Marehemu Omary Maunda.Omary Maunda amefariki kwa ugonjwa wa kupungukiwa damu mara kwa mara mwilini
Askari wenye vyeo vya Afisa mkaguzi msaidizi wa Magereza wakiwa wamebeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Omary Maunda ambae mpaka anakufa alikua na Cheo cha Afisa Mkaguzi Msaidizi wa Mgereza. Omary Maunda ameacha Mke na mtoto mmoja.
Askari Magereza wakipokea Mwili wa Askari mwenzao Marehemu Omary Maunda kutoka kwa Waumini wa dini ya Kiislam waliokuwa wameubeba kwa ajili ya kupisha taratibu za mazishi za kijeshi kuendelea
Askari wa Jeshi la Magereza wakipiga Risasi Hewani kama Ishara ya Heshima kwa askari mwenzao aliefariki dunia Marehemu Omary Maunda ambae alikua ni mwanafunzi wa zamani wa Ununio Boys High School.
No comments:
Post a Comment