TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Wednesday, April 25, 2012

Mwamuzi... mechi ya Azam achanwa mdomo, amtaja Sued

MWAMUZI wa kati aliyechezesha mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Azam na Mtibwa Sugar, juzi, alichanwa mdomo na kumtaja Salum Sued ndiye aliyempiga ngumi. Mwamuzi huyo, Rashidi Msangi, wa Mpwapwa, amemtaja nahodha huyo wa Mtibwa Sugar kuwa ndiye aliyempiga ngumi na kumchana mdomo. Tukio hilo lilitokea dakika ya 88 baada ya wachezaji wa Mtibwa Sugar kugomea mkwaju wa penalti ambao Azam ilipewa wakati timu hizo zikiwa sare ya bao 1-1 kwa madai kuwa haikuwa halali. Fujo hizo zilizuiwa na Jeshi la Polisi ambalo lilimuokoa mwamuzi huyo na kumpeleka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, lakini jitihada hizo hazikufanikiwa baada ya wachezaji kumfuata nyuma huku wakimrushia chupa za maji mgongoni. Akizungumza na Championi Jumatatu, mara baada ya kuvunja mechi hiyo, Msangi alisema wachezaji wote wa Mtibwa Sugar walimzonga lakini Swed ndiye aliyempiga ngumi mdomoni. “Wewe ukiwa mwandishi unaonaje? Ile ni penalti au? Kwangu nimeona ni sahihi kwani mchezaji wao ameshika ndani ya sita ndiyo maana nikapuliza filimbi. “Sasa nashangaa wananizonga kunifanyia fujo na nahodha wao (Sued) amenipiga ngumi ya mdomo, angalia mwenyewe nilivyochanika na kuvimba,” alisema Msangi. Hili ni tukio la pili kwa mwamuzi kupigwa kwenye mchezo unaohusisha timu ya Azam. Mchezo wa kwanza ulikuwa kati ya Azam na Yanga ambao wachezaji wa Yanga, walimpiga mwamuzi Israel Nkongo baada ya kumpa kadi nyekundu Haruna Niyonzima na kupigwa ngumi na Stephano Mwasyika.

No comments: