TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Saturday, November 26, 2011

TUNAWEZA KUUONDOA UKATILI WA JINSIA NCHINI. WANAWAKE SHIKA HATAMU LETA MABADILIKO


"Picha ya Juu jamaa akimpeleka mkewe hospitali huku akiwa kambeba mgongoni mara baada ya kukosa fedha ya usafiri.Picha ya Chini Jamaa aliefahamika kwa jina la Kwingwa Mhina wa Kigogo Luhanga akimpiga mkewe mara baada ya kuhitilafiana"

Asilimia 47 ya wanawake wanakubali kwamba mume ana haki ya kumpiga mkewe pale mwanamke anapozembea kuangalia watoto.

Aidha asilimia 29 wanakubali kwamba mume ana haki ya kumpiga mkewe iwapo atakataa kufanya tendo la ndoa na asilimia 20 watapigwa ikiwa wataunguza chakula.

Taarifa hiyo imo katika hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa niaba ya Naibu Waziri wa wizara hiyo, Kijakazi Mtengwa aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizofanyika ukumbi wa Don Bosco, Dar es Salaam jana.

Mtengwa alisema takwimu hizo kutoka utafiti uliofanywa mwaka 2010 na Idara ya Takwimu kuhusu hadhi ya wanawake nchini ulibaini pia asilimia 46 ya wanawake wanaafikia kwamba mume ana haki ya kumpiga mkewe iwapo mke atajibishana naye, asilimia 43 ya wanawake wanaafiki mume ana haki ya kumpiga mkewe kwa sababu ya kuondoka bila kuaga, “Hizi ni fikra potofu kwa wanawake na wanaume na zinapaswa kupingwa kwa nguvu zote, Serikali kwa kushirikiana na wadau wake wa maendeleo inafanya jitihada mbalimbali katika kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto,” alisema.

Alisema katika kupambana na tatizo la ukatili wa kijinsia zipo mbinu mbalimbali zinazoweza kutumiwa ili kusonga mbele katika kufikia malengo ikiwa ni pamoja na kutumia mbinu shirikishi jamii ili kuhakikisha kunakuwa na ushiriki wa makundi yote katika jamii, kwa kutumia mbinu hizi wananchi wataweza kubuni mikakati ya kijamii ambayo ndiyo italeta suluhisho la kudumu la tatizo hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake katika sheria na Maendeleo Afrika (Wildaf), Naomi Kaihula alisema vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake sio tu kwamba vinadhoofisha kiafya, bali pia vinaathiri uwezo wao wa kushiriki na kuchangia katika kuleta maendeleo kiuchumi ndani ya familia zao na nchi.

Takwimu nyingine zinaonyesha kuwa makosa ya ubakaji yamekuwa yakiongezeka kutoka 3,721 mwaka 2002 na kufikia 8,878 mwaka 2007 wakati huo makosa ya ulawiti yaliongezeka kutoka 490 mwaka 2002 kufikia 567 mwaka 2007.

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Kweli inabidi mabadiliko kama hizo nambo ni kweli duh!