TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Tuesday, November 8, 2011

MBOWE, SLAA, LISSU: NI MKESHA WA SIKU 7

Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiwa katika viwanja vya NMC jijini Arusha jana.

Ni baada ya Lema kubakia tena mahabusu -Jiji la Arusha larindima, umati wajaa NMCMAELFU ya wakazi wa Jiji la Arusha, jana walikubali kunyeshewa mvua katika mkutano wa hadhara ambapo viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), walitangaza mkesha wa ukombozi hadi hapo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, atakapopewa dhamana.Aidha, wamesema mkesha wa aina hiyo utaendelea kwa mikoa ya Mwanza, Mbeya na Kilimanjaro huku mkoa wa Dar es Salaam ukijiandaa kwa harakati hizo.Akitangaza kuwepo kwa mkesha huo huku mvua ikinyesha, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa alisema: “Uwanja huu utakuwa mali ya wakazi wa Arusha, na sisi hatutatoka hapa mpaka Lema atakapotoka mahabusu.”Mvua ilianza kunyesha majira ya saa 9:30 alasiri hivi hadi saa 11:00 jioni, lakini haikuwafanya mamia kwa maelfu ya wafuasi hao wa Chadema kukimbia eneo hilo.Mkesha huo ulitangazwa saa chache baada ya harakati za kumtoa Lema kwa kumwekea dhamana, ili atoke mahabusu kukwama baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kusema anatakiwa apelekwe mahakamani hapo, Novemba 14, mwaka huu, saa 2: 30 asubuhi.Msimamo huo ulitolewa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Richard Magessa, akijibu ombi la Wakili wa Lema, Method Kimomogoro, aliyeiomba itoe hati ya kumtoa Lema mahabusu na kumleta mahakamani hapo kwa ajili ya kumwekea dhamana.Katika barua ya mahakama hiyo yenye kumbukumbu namba RM/GC/Vol III/50 ya Novemba 7, 2011, ilisema: “Wadhamini wa mshtakiwa wafike mahakamani siku ya kutajwa kesi, 14/11/2011, saa 2:30 asubuhi kwa ajili ya utaratibu wa dhamana.”Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, Dk. Slaa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, walifika mahakamani hapo kufuatilia taratibu za kumtoa Lema.Hata hivyo, baada ya kupata taarifa hiyo, Mbowe, alilazimika kuwatuliza maelfu ya wananchi wa Arusha waliokusanyika nje ya viwanja vya mahakama kwamba watulie, kwa kuwa Chadema ni chama chenye nidhamu.Alisema wameanzisha mapambano ya historia ya taifa hili, kwamba ukombozi wa Tanzania utaanzia hapa: “Tupo kwenye maombolezo kwa sababu mbunge mliyemchagua na kushinda kwa kura nyingi zaidi ya 20,000 amekuwa akinyanyaswa tangu alipochaguliwa, na hii inamaanisha kwamba ninyi mliomchagua hamna maana.”Alisema anataka umati huo upeleke ujumbe kwa chama tawala na serikali yake kwamba hakuna mwenye hatimiliki ya nchi hii.“Sisi sote tumezaliwa hapa, tunaishi hapa na tutakufa hapa na hakuna mwenye hatimiliki ya maisha ya mtu mwingine…tusije tukalaumiwa kwa kuchukua maamuzi haya magumu, hii inatokana na CCM yenyewe kutulazimisha kuchukua maamuzi haya,” alisema muda mfupi kabla ya kutangaza kuanza kwa mkesha.Akitangaza utaratibu wa mkesha huo, Mbowe, alisema: “Sasa hivi hatutazungumza lugha ya Lema, tunazungumza lugha ya ukombozi.”Alisema matatizo ya Arusha yalianza tangu uchaguzi wa Meya ambao alisema CCM iliuvurunda na kwamba Meya aliyechaguliwa ni batili.Alisema suala hilo lilifikishwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye alimwandikia barua Katibu Mkuu wa Chadema, lakini hakuna ufumbuzi wowote ambao umefikiwa hadi sasa.“CCM wanaringa kuwa wana polisi, wana magereza, wana risasi, wana mabomu…sasa nawaambia kwamba hatuogopi mvua na tutakesha hapa tuzungumze kuhusu masuala ya ukombozi,” alisema na kuongeza: “Tumeanza mbinu mpya ya mapambano, hivyo, kama viongozi tumeamua tutakesha katika viwanja hivi hadi hapo serikali itakapoamua kutuletea mbunge wetu.”Alisema mkesha huo hauwahusu watoto wadogo kwa kuwa ‘ngoma’ hiyo ni nzito kwao na hivyo akawataka warudi majumbani kwao kulala na kuwaacha hapo watu wakubwa.“Hatuwezi kuendelea kujenga taifa la watu wenye woga, watu ambao wanatishwa na wenzao,” alisema na kuongeza: “Tunaposema hakuna kulala mpaka kieleweke naona watu hawatuelewi.”Alisisitiza kuwa mkesha huo ni wa ukombozi na hawezi kuufunga mkutano huo kwa sababu wameamua kukesha kwa amani.Aliusihi umati huo kuacha kuleta vurugu, kumpiga mtu wala kusukumana ili watu wasiowapenda wasipate sababu ya kuwajengea hoja kwamba chama hicho ni cha watu wasio na nidhamu.“Wakitaka kutupiga, waje watupige na wakitaka kutupakia kwenye magari waje watupakie na kutupeleka kwa mahabusu, hatuogopi kabisa,” alisema.ATULIZA HALI MAHAKAMANIAwali, Mbowe alitumia busara ya ziada kuwatuliza wafuasi wa Chadema waliokuwa wamefurika mahakamani kumsubiri Lema.“Makamanda naomba muwe watulivu, Chadema ni chama chenye nidhamu, kwa kuwa kesi zingine zinaendelea mahakamani hapa, naomba twende viwanja wa NMC ambako tutawaelezeni kila kitu kilichojiri….mimi kamanda wenu pamoja na Dk. Slaa na Tundu Lissu tutaongoza maandamano hayo hadi viwanja vya NMC,” alisema huku akishangiliwa na umati huo wa watu.Mapema wakati Mbowe alipowasili mahakamani hapo, majira ya saa 8:51 mchana na kuingia ndani ya viwanja vya mahakama, kundi kubwa la wafuasi wa Chadema waliokuwa wamesimama tangu asubuhi nje ya uzio wa mahakama, waliingia ndani wakimsindikiza.Hali hiyo iliwafanya polisi wa kutuliza ghasia waliokuwa kwenye Land Rover yenye namba za usajili PT 1178 kuendesha gari lao kwa kasi kwa lengo la kuzuia gari la Mbowe, aina ya Toyota lenye namba za usajili T968 BRH, lisisonge mbele zaidi kuelekea mahakamani.Baada ya kuzuiwa Mbowe alishuka kwenye gari lake na baada ya kuzungumza kwa muda na askari polisi, aliwaomba wafuasi wake kwamba watoke nje ya viwanja hivyo.“Nimekuja hapa kushughulikia suala hili la Lema, naomba msilete vurugu, Chadema ni chama chenye nidhamu, au sio makamanda, sasa nawaomba mtoke nje ya viwanja kwa kuwa kuna kesi za watu zinaendelea mahakamani hapa, tuwape utulivu ili kesi zao zipate kusikilizwa kwa haki,” alisema.Baada ya kusema hayo wafuasi hao walitii amri hiyo na kutoka nje ambako waliendelea kusubiri hadi majira ya 9:20, walipopata taarifa ya kutakiwa kwenda viwanja vya NMC kwenye mkutano.Aidha, maelfu ya watu waliojitokeza mahakamani hapo walikuwa na shauku ya kutaka kumwona mbunge wao akitolewa mahabusu na pia umati kama huo ulikuwepo Kisongo, kona ya kwenda magereza wakimsubiri Lema atolewe.Watu hao wote waliokuwepo mahakamani hapo na wale waliokuwepo eneo la Kisongo nao pia walitembea kwa miguu hadi kwenye viwanja vya NMC kusikiliza mkutano ili kujua kulikoni.MAHABUSU WAGOMA KUSHUKA KWENYE KARANDINGAMapema majira ya saa 4 asubuhi karandinga la polisi lililokuwa limewabeba mahabusu kusikiliza kesi zao, waligoma kuteremka kwenye gari hilo, lakini mahabusu wachache wanawake waliteremka.Baada ya kuwasubiri kwa zaidi ya robo saa bila kuteremka, askari polisi waliowaleta waliamua kuwarejesha gerezani, pamoja na mahabusu wanawake ambao awali walishuka kwenye karandinga hilo.Wakigoma kushuka kwenye karandinga hilo, mahabusu hao walisikika wakisema kwa sauti kubwa kwamba hawashuki hadi Lema atakapoletwa mahakamani hapo.Maneno hayo yaliwafanya polisi kuwaamuru mahabusu wa kike walioteremka kupanda kwenye gari na wote wakarudishwa gerezani Kisongo.Umati wa watu ulizidi kufurika katika viwanja vya mahakama, lakini idadi kubwa zaidi ya watu ilibaki nje ya uzio wa mahakama ambako walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kuhamasishana.Baadhi ya nyimbo walizokuwa wakiimba ni ‘Lema usiogope…usiogope magereza Lema,’ na wakati fulani ofisa mmoja wa polisi aliyekuwa kwenye gari aina ya Landrover lenye namba za usajili PT 1844 aliwaomba wafuasi hao wa Chadema kutangulia kwenye viwanja vya NMC ambako chama hicho kilipanga kufanya mkutano mkubwa wa hadhara, lakini walikataa na kisha akaambulia kuzomewa.Watu hao walikuwa wameshika bendera na matawi ya miti wakipeperusha juu huku wakirukaruka na kuendelea kuimba nyimbo mbalimbali.Kila lilipokuwa likipita gari la polisi, walisikika wakiimba Chadema semaaa…sema usigope semaa, Lema semaa…semaaa usiogope, semaa…sisi mapanya hatuogopi magereza, sema.Mbwembwe za kuzunguka na pikipiki aina ya Toyo zilizokuwa na bendera za chama zilitoa burudani ya kutosha nje ya uzio wa mahakama hali ambayo iliwafanya wasichoke.Wakati fulani majira yaa 6 hivi mchana, mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Wilaya ya Arumeru, Nelson Nassari, alilazimika kuwatuliza vijana hao na kuwaeleza kwamba taratibu ndio zinazochelewesha kumtoa Lema, lakini aliwaeleza matumaini yake kwamba angetoka jana.Alisema taratibu hizo zinafanywa kwa makusudi ili kuchelewesha muda wa saa 5 walioomba kufanya mkutano katika viwanja vya NMC.Akiwatuliza alisema anatoa muda wa nusu saa na baada ya kupita muda huo kama taratibu za kupata hati ya kumtoa Lema mahabusu itachelewa, basi atawaruhusu waingie ndani ya uzio wa mahakama.Palikuwa hapatoshi mahakamani kwa mbwembwe za vijana hao ambao walizidi kuimba nyimbo za kutiana hamasa na kila mara gari la polisi lilipokuwa likipita vijana hao walisikika wakiimba, ’polisi hatutaki unyanyasaji, hatumtaki huyo Zuberi (Zuberi Mwombeji ni Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Arusha).Pia walikuwa wakiimba, “Said Mwema mkanye Zuberi” na wakati mwingine walikuwa wakisikika kuimba, “Tumeyamisi mabomu ya polisi.” Nyimbo zingine ni kama “Mmetuita panya, nyie ni manyau.”Vijana hao wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, ‘kama tatizo ni ubunge apewe Zuberi na u-OCD apewe Lema.Hali ya mitaa mbalimbali jijini hapa ilijaa kila aina ya mbwembwe ya misafara ya pikipiki na magari yaliyokuwa na bendera za Chadema, na idadi kubwa ya watu ilikuwa tayari imefurika katika viwanja vya NMC kuanzia majira ya saa 4 asubuhi.Watu wengi walikwenda kumsubiri Lema eneo la Kisongo wakiwa kwenye pikipiki na magari hali ambayo ilivuta umati mkubwa wa watu.CHANZO: NIPASHEViongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiwa katika viwanja vya NMC jijini Arusha jana. -Ni baada ya Lema kubakia tena mahabusu -Jiji la Arusha larindima, umati wajaa NMCMAELFU ya wakazi wa Jiji la Arusha, jana walikubali kunyeshewa mvua katika mkutano wa hadhara ambapo viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), walitangaza mkesha wa ukombozi hadi hapo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, atakapopewa dhamana.Aidha, wamesema mkesha wa aina hiyo utaendelea kwa mikoa ya Mwanza, Mbeya na Kilimanjaro huku mkoa wa Dar es Salaam ukijiandaa kwa harakati hizo.Akitangaza kuwepo kwa mkesha huo huku mvua ikinyesha, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa alisema: “Uwanja huu utakuwa mali ya wakazi wa Arusha, na sisi hatutatoka hapa mpaka Lema atakapotoka mahabusu.”Mvua ilianza kunyesha majira ya saa 9:30 alasiri hivi hadi saa 11:00 jioni, lakini haikuwafanya mamia kwa maelfu ya wafuasi hao wa Chadema kukimbia eneo hilo.Mkesha huo ulitangazwa saa chache baada ya harakati za kumtoa Lema kwa kumwekea dhamana, ili atoke mahabusu kukwama baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kusema anatakiwa apelekwe mahakamani hapo, Novemba 14, mwaka huu, saa 2: 30 asubuhi.Msimamo huo ulitolewa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Richard Magessa, akijibu ombi la Wakili wa Lema, Method Kimomogoro, aliyeiomba itoe hati ya kumtoa Lema mahabusu na kumleta mahakamani hapo kwa ajili ya kumwekea dhamana.Katika barua ya mahakama hiyo yenye kumbukumbu namba RM/GC/Vol III/50 ya Novemba 7, 2011, ilisema: “Wadhamini wa mshtakiwa wafike mahakamani siku ya kutajwa kesi, 14/11/2011, saa 2:30 asubuhi kwa ajili ya utaratibu wa dhamana.”Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, Dk. Slaa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, walifika mahakamani hapo kufuatilia taratibu za kumtoa Lema.Hata hivyo, baada ya kupata taarifa hiyo, Mbowe, alilazimika kuwatuliza maelfu ya wananchi wa Arusha waliokusanyika nje ya viwanja vya mahakama kwamba watulie, kwa kuwa Chadema ni chama chenye nidhamu.Alisema wameanzisha mapambano ya historia ya taifa hili, kwamba ukombozi wa Tanzania utaanzia hapa: “Tupo kwenye maombolezo kwa sababu mbunge mliyemchagua na kushinda kwa kura nyingi zaidi ya 20,000 amekuwa akinyanyaswa tangu alipochaguliwa, na hii inamaanisha kwamba ninyi mliomchagua hamna maana.”Alisema anataka umati huo upeleke ujumbe kwa chama tawala na serikali yake kwamba hakuna mwenye hatimiliki ya nchi hii.“Sisi sote tumezaliwa hapa, tunaishi hapa na tutakufa hapa na hakuna mwenye hatimiliki ya maisha ya mtu mwingine…tusije tukalaumiwa kwa kuchukua maamuzi haya magumu, hii inatokana na CCM yenyewe kutulazimisha kuchukua maamuzi haya,” alisema muda mfupi kabla ya kutangaza kuanza kwa mkesha.Akitangaza utaratibu wa mkesha huo, Mbowe, alisema: “Sasa hivi hatutazungumza lugha ya Lema, tunazungumza lugha ya ukombozi.”Alisema matatizo ya Arusha yalianza tangu uchaguzi wa Meya ambao alisema CCM iliuvurunda na kwamba Meya aliyechaguliwa ni batili.Alisema suala hilo lilifikishwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye alimwandikia barua Katibu Mkuu wa Chadema, lakini hakuna ufumbuzi wowote ambao umefikiwa hadi sasa.“CCM wanaringa kuwa wana polisi, wana magereza, wana risasi, wana mabomu…sasa nawaambia kwamba hatuogopi mvua na tutakesha hapa tuzungumze kuhusu masuala ya ukombozi,” alisema na kuongeza: “Tumeanza mbinu mpya ya mapambano, hivyo, kama viongozi tumeamua tutakesha katika viwanja hivi hadi hapo serikali itakapoamua kutuletea mbunge wetu.”Alisema mkesha huo hauwahusu watoto wadogo kwa kuwa ‘ngoma’ hiyo ni nzito kwao na hivyo akawataka warudi majumbani kwao kulala na kuwaacha hapo watu wakubwa.“Hatuwezi kuendelea kujenga taifa la watu wenye woga, watu ambao wanatishwa na wenzao,” alisema na kuongeza: “Tunaposema hakuna kulala mpaka kieleweke naona watu hawatuelewi.”Alisisitiza kuwa mkesha huo ni wa ukombozi na hawezi kuufunga mkutano huo kwa sababu wameamua kukesha kwa amani.Aliusihi umati huo kuacha kuleta vurugu, kumpiga mtu wala kusukumana ili watu wasiowapenda wasipate sababu ya kuwajengea hoja kwamba chama hicho ni cha watu wasio na nidhamu.“Wakitaka kutupiga, waje watupige na wakitaka kutupakia kwenye magari waje watupakie na kutupeleka kwa mahabusu, hatuogopi kabisa,” alisema.ATULIZA HALI MAHAKAMANIAwali, Mbowe alitumia busara ya ziada kuwatuliza wafuasi wa Chadema waliokuwa wamefurika mahakamani kumsubiri Lema.“Makamanda naomba muwe watulivu, Chadema ni chama chenye nidhamu, kwa kuwa kesi zingine zinaendelea mahakamani hapa, naomba twende viwanja wa NMC ambako tutawaelezeni kila kitu kilichojiri….mimi kamanda wenu pamoja na Dk. Slaa na Tundu Lissu tutaongoza maandamano hayo hadi viwanja vya NMC,” alisema huku akishangiliwa na umati huo wa watu.Mapema wakati Mbowe alipowasili mahakamani hapo, majira ya saa 8:51 mchana na kuingia ndani ya viwanja vya mahakama, kundi kubwa la wafuasi wa Chadema waliokuwa wamesimama tangu asubuhi nje ya uzio wa mahakama, waliingia ndani wakimsindikiza.Hali hiyo iliwafanya polisi wa kutuliza ghasia waliokuwa kwenye Land Rover yenye namba za usajili PT 1178 kuendesha gari lao kwa kasi kwa lengo la kuzuia gari la Mbowe, aina ya Toyota lenye namba za usajili T968 BRH, lisisonge mbele zaidi kuelekea mahakamani.Baada ya kuzuiwa Mbowe alishuka kwenye gari lake na baada ya kuzungumza kwa muda na askari polisi, aliwaomba wafuasi wake kwamba watoke nje ya viwanja hivyo.“Nimekuja hapa kushughulikia suala hili la Lema, naomba msilete vurugu, Chadema ni chama chenye nidhamu, au sio makamanda, sasa nawaomba mtoke nje ya viwanja kwa kuwa kuna kesi za watu zinaendelea mahakamani hapa, tuwape utulivu ili kesi zao zipate kusikilizwa kwa haki,” alisema.Baada ya kusema hayo wafuasi hao walitii amri hiyo na kutoka nje ambako waliendelea kusubiri hadi majira ya 9:20, walipopata taarifa ya kutakiwa kwenda viwanja vya NMC kwenye mkutano.Aidha, maelfu ya watu waliojitokeza mahakamani hapo walikuwa na shauku ya kutaka kumwona mbunge wao akitolewa mahabusu na pia umati kama huo ulikuwepo Kisongo, kona ya kwenda magereza wakimsubiri Lema atolewe.Watu hao wote waliokuwepo mahakamani hapo na wale waliokuwepo eneo la Kisongo nao pia walitembea kwa miguu hadi kwenye viwanja vya NMC kusikiliza mkutano ili kujua kulikoni.MAHABUSU WAGOMA KUSHUKA KWENYE KARANDINGAMapema majira ya saa 4 asubuhi karandinga la polisi lililokuwa limewabeba mahabusu kusikiliza kesi zao, waligoma kuteremka kwenye gari hilo, lakini mahabusu wachache wanawake waliteremka.Baada ya kuwasubiri kwa zaidi ya robo saa bila kuteremka, askari polisi waliowaleta waliamua kuwarejesha gerezani, pamoja na mahabusu wanawake ambao awali walishuka kwenye karandinga hilo.Wakigoma kushuka kwenye karandinga hilo, mahabusu hao walisikika wakisema kwa sauti kubwa kwamba hawashuki hadi Lema atakapoletwa mahakamani hapo.Maneno hayo yaliwafanya polisi kuwaamuru mahabusu wa kike walioteremka kupanda kwenye gari na wote wakarudishwa gerezani Kisongo.Umati wa watu ulizidi kufurika katika viwanja vya mahakama, lakini idadi kubwa zaidi ya watu ilibaki nje ya uzio wa mahakama ambako walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kuhamasishana.Baadhi ya nyimbo walizokuwa wakiimba ni ‘Lema usiogope…usiogope magereza Lema,’ na wakati fulani ofisa mmoja wa polisi aliyekuwa kwenye gari aina ya Landrover lenye namba za usajili PT 1844 aliwaomba wafuasi hao wa Chadema kutangulia kwenye viwanja vya NMC ambako chama hicho kilipanga kufanya mkutano mkubwa wa hadhara, lakini walikataa na kisha akaambulia kuzomewa.Watu hao walikuwa wameshika bendera na matawi ya miti wakipeperusha juu huku wakirukaruka na kuendelea kuimba nyimbo mbalimbali.Kila lilipokuwa likipita gari la polisi, walisikika wakiimba Chadema semaaa…sema usigope semaa, Lema semaa…semaaa usiogope, semaa…sisi mapanya hatuogopi magereza, sema.Mbwembwe za kuzunguka na pikipiki aina ya Toyo zilizokuwa na bendera za chama zilitoa burudani ya kutosha nje ya uzio wa mahakama hali ambayo iliwafanya wasichoke.Wakati fulani majira yaa 6 hivi mchana, mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Wilaya ya Arumeru, Nelson Nassari, alilazimika kuwatuliza vijana hao na kuwaeleza kwamba taratibu ndio zinazochelewesha kumtoa Lema, lakini aliwaeleza matumaini yake kwamba angetoka jana.Alisema taratibu hizo zinafanywa kwa makusudi ili kuchelewesha muda wa saa 5 walioomba kufanya mkutano katika viwanja vya NMC.Akiwatuliza alisema anatoa muda wa nusu saa na baada ya kupita muda huo kama taratibu za kupata hati ya kumtoa Lema mahabusu itachelewa, basi atawaruhusu waingie ndani ya uzio wa mahakama.Palikuwa hapatoshi mahakamani kwa mbwembwe za vijana hao ambao walizidi kuimba nyimbo za kutiana hamasa na kila mara gari la polisi lilipokuwa likipita vijana hao walisikika wakiimba, ’polisi hatutaki unyanyasaji, hatumtaki huyo Zuberi (Zuberi Mwombeji ni Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Arusha).Pia walikuwa wakiimba, “Said Mwema mkanye Zuberi” na wakati mwingine walikuwa wakisikika kuimba, “Tumeyamisi mabomu ya polisi.” Nyimbo zingine ni kama “Mmetuita panya, nyie ni manyau.”Vijana hao wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, ‘kama tatizo ni ubunge apewe Zuberi na u-OCD apewe Lema.Hali ya mitaa mbalimbali jijini hapa ilijaa kila aina ya mbwembwe ya misafara ya pikipiki na magari yaliyokuwa na bendera za Chadema, na idadi kubwa ya watu ilikuwa tayari imefurika katika viwanja vya NMC kuanzia majira ya saa 4 asubuhi.Watu wengi walikwenda kumsubiri Lema eneo la Kisongo wakiwa kwenye pikipiki na magari hali ambayo ilivuta umati mkubwa wa watu.


No comments: