TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Sunday, October 30, 2011

WEMA SEPETU ANUSURIKA KIFO

Mdada wa nguvu Wema Sepetu.

WEMA Isaac Sepetu, Jumatano iliyopita ilikuwa siku ngumu mno kwake na kama si jitihada za mzazi, leo yangekuwa yanazungumzwa mengine.

Wema ambaye hana historia ya kumlilia mwanaume, amekamatika kwenye penzi la brazameni anayedatisha ‘maduu’, Naseeb Abdul ‘Diamond’, Jumatano iliyopita baada ya kuambiwa anaachwa, aliona bora ajisalimishe kaburini kwa kunywa sumu.

Busara za mama mzazi wa Diamond, Sanura Khassim ‘Sandra’ ziliokoa jahazi kwa kumlazimisha mwanaye arudiane na Wema ili mambo yasiharibike.

WEMA ALIVYODATA
Jumatano iliyopita mchana, Wema alipata taarifa kuwa Diamond ‘Platinumz’ alishazungumza na waandishi wa habari na kuwaeleza uamuzi wake wa kumuacha jumla.

Wema ambaye ni Miss Tanzania 2006-07, alipata taarifa hizo akiwa kwenye kambi ya kurekodi filamu kwenye Hoteli ya Lamada, Ilala, Dar es Salaam.

Tukio la kwanza, Wema alivua pete ya uchumba aliyovalishwa na Diamond kwa hasira, akaanza kulia.
Baada ya kutafakari, Wema aliona mtetezi pekee ni mama mkwe wake, Sandra, hivyo alimpigia simu na kuangusha kilio cha “mama mkwe nisaidie mwanao asiniache.”

Utu uzima dawa, Sandra alimwita mrembo huyo nyumbani kwake, Sinza, Dar ili wazungumze. Mapenzi ya Diamond ndani ya Wema, yana nguvu kuliko kazi, kwa hiyo akaondoka kambini bila kurekodi na kumuacha prodyuza wa muvi hiyo, Suleiman Barafu akiwa na mshangao.

Barafu alikasirika lakini wasanii wenzake, walimshauri amvumilie Wema kwa sababu yupo kwenye mateso makubwa ya kimapenzi.
Wema alipofika nyumbani, alimvamia mama mkwe wake, ‘mchozi’ huo, akamlamba miguu, akasema: “Mama nampenda Diamond kuliko chochote, akiniacha sina pa’ kuweka sura yangu.”

Akamchanganya mama mkwe: “Sitanii mama, endapo Diamond ataniacha, sitakuwa na uwezo wa kubeba haya mapenzi makubwa niliyonayo. Nitakunywa sumu, nitakufa. Ila sitajali kwa sababu nitakufa kwa sababu ya penzi la mwanaume ninayempenda.”