TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Saturday, October 8, 2011

SABABU KUU ZA KUSHINDWA CHADEMA KATIKA UCHAGUZI WA IGUNGA KATIKA PICHA

1. UKOSEFU WA ELIMU YA URAIA,KUTOKUJUA KUSOMA NA KUANDIKA,USHAMBA NA UJINGA WA VIJANA WENGI WA CHADEMA



Kura nyingi zilizoharika Igunga karibu 88% ni za CHADEMA. Na nyingi ya kura hizo ziliandikwa Matusi, majina ya watu na Sahihi kama inavyoonekana katika Picha. Wakati umefika sasa kwa CHADEMA kuanza zoezi la kutoa elimu ya Uraia kwa Wanachama wake nasio kutumia hela nyingi katika Kampeni na kusahau Elimu ya Uraia.

2. MAWAKALA WA CHADEMA HAWAKUANDALIWA VIZURI KISAIKOLOJIA


Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni akiwawezesha Mawakala wa CHADEMA namna ya kulinda kura siku moja kabla ya uchaguzi wa Igunga Kufanyika.Maizngira ya Warsha hiyo ni kama yanavyoonekana hapo ni bara barani katika ofisi ya CHADEMA wilaya Igunga.Maandalizi haya hayakuwa mazuri na mawakala hawakuandaliwa vema kushiriki kulinda kura.

3.MAWAKALA WA CHADEMA HAWAKUWA MAKINI.



Kwenye baadhi ya vituo mawakala wa CHADEMA hawakuwa makini kiasi cha kuwaachia uhuru wasimamizi wa Uchaguzi kufanya wanavyotka katika zoezo la kupiga kura hadi kuhesabu kama inavyoonekana katika Picha.

4. KUWEPO KWA ASKARI WA DORIA VITUONI

Askari polisi waliokuwa wanzunguka ovyo mitaani walichangia kuwaogopesha wapiga kura mbali mbali haswa vijana.Watu wengi walishindwa kujitokeza kupiga kura kwa sababu hiyo ya hofu ya kuvunjika kwa amani.

5. UMBALI KUTOKA KITUO KIMOJA HADI KINGINE

Vituo vingi vya kupigia kura vilikua mbali mbali sana Karibu Kilometa 20 hadi 30 hivyo kuwafanya Vijana wengi wasijitokeze Kupi kura.

6. MVUA KUBWA ILIONYESHA.

Mvua Kubwa iliokua ikinyesha iliwafanya vijana wengi wasipige kura na badala yake wazee na akina mama wengi walijitokeza kupiga kura kwa wingi.

7. RUSHWA
Baadhi ya watendaji wa Vijiji na kata walitumika kutoa Rushwa ya Mahindi, Pesa na Chumvi ili kuiangamiza CHADEMA.

No comments: