TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Sunday, September 11, 2011

PICHA ZA MATUKIO YA UOKOAJI KATIKA AJALI YA MELI YA ZANZIBAR


Wakazi wa kisiwa cha Unguja wakishirikiana na Wanajeshi katika zoezi la uokoaji wa watu walionusurika na Maiti wa ajali ya Meli ya Mv Spice
Mmoja wa Watalii wa Visiwa vya Unguja akimfariji mmoja ya watoto walionusurika katika ajali ya Mv Spice iliotokea usiku wa kuamkia jana.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akitoa maelezo ya namna ajali ya meli ya mv Spice ilivotokea kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal akimfariji moja ya wananchi waliokoka katika ajali ya meli ya Mv Islanders
Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akiwa katika kikao cha dharula wengine katika Ikulu ya Wete mjini Pemba

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Rais wz Zanzibar Dr.Ally Mohammed Shein na viongozi wengie wakiwa na nyuso za majonzi wakati wakielekea kutoa salamu za rambi rambi kwa wananchi wa visiwa vya Unguja

Wakazi wa Visiwa wa Unguja wakiwa katika taratibu za kutambua na kubeba miili ya watu waliokufa katika ajali ya meli ya Mv Spice iliotokea usiku wa kuamkia jana katika pwani ya mkondo wa Nungwi.

Baadhi ya Abiria waliosalimika wakiwa wamejipumzisha mara baada ya kuokolewa

Mmoja ya wakazi wa Mjini Unguja akiwa amebeba moja ya maiti ya ajali ya meli ya Spice Islander.

No comments: