TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Sunday, August 7, 2011

MADIWANI 6 HATARINI KUVULIWA UDIWANI CHADEMA


Madiwani sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wameitwa na Kamati Kuu ya chama hicho mjini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa kuhusiana na uamuzi wao wa kukubali muafaka wa umeya katika Jiji Arusha bila ridhaa ya chama chao.

Bloh hii ilishuhudia madiwani hao wakiranda randa nje ya ukumbi huo hadi saa 12:00 jioni wakisubiri kuitwa kuhojiwa katika kikao hicho.

Kikao hicho kilichoketi jana chini ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kiliwaita madiwani hao mjini Dodoma kwa ajili ya kuwahoji.

Hata hivyo, vyanzo vya habari vilisema kuwa lengo la chama ni kuhoji diwani mmoja mmoja, jambo ambalo lilipingwa na madiwani hao waliotaka kuingia wote kwa wakati mmoja katika kikao hicho kwa ajili ya kuhojiwa.

Madiwani waliofika ni Naibu Meya wa jiji hilo na diwani wa kata ya Kimandolu, Estomii Malla, John Bayo (Elerai), Charles Mtanda (Kaloleni), Reuben Ngowi (Themi), Rehema Mohamed (Viti Maalum).

Madiwani watano kati ya 11 walikubali kukiomba radhi chama chao wakati watano walikataa kuomba radhi chama chao kwa kitendo cha kuingia katika muafaka kati yao na madiwani wa CCM, bila ridhaa ya chama.

No comments: