TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Thursday, June 30, 2011

SAU YAISHANGAA UDOM

Mkurugenzi wa vijana wa chama cha siasa cha SAU(SAUTI YA UMMA)ndugu Christopher Robert Kajituel ameongea na blog na kusema kwamba anaushangaa uongozi wa chuo cha UDOM baada ya kudai kwamba wanafunzi waliorudishwa nyumbani baada ya mgomo ni wafuasi wa vyama vya upinzani.

Huku akizidi kufafanua juu ya suala hili,kiongozi huyu wa SAU alienda mbali zaidi kwa kuishangaa serikali kwa kuminya haki na demokrasia ya watanzania pale wanapoandamana kudai haki zao."Namshangaa pia mkuu wa wilaya aliyenukuliwa na gazeti la Mwananchi la tarehe 27.6.2011 aliyesema eti moja ya sharti la kuwarudisha chuoni wanafunzi hao ni lazima wawe CCM.Inaelekea hajui sheria,moja ya njia za kudai haki yako ni kuandamana...Mkuu wa wilaya huyu ni dikteta.SAU hatumsapoti."

SAU imeamua kuwapigania wanachuo wa UDOM ili warudi darasani ili waje waijenge Tanzania mpya na wanafanya mawasiliano na mwanasheria wao.MUNGU ibariki SAU.

Habari na mda ALLAN HALID KILUVIA.

No comments: