TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Tuesday, May 24, 2011

VIONGOZI WA CHADEMA MBARONI TARIMEVIONGOZI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO WATIWA MBARONI TARIME:

Viongozi wa chama cha CHADEMA wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayai Tarime kufuatia hatua ya Jeshi la Polisi kutaka Kuiteka miili ya Marehemu waliokufa kufuatia vurugu zilizotokea katika mgodiwa Nyamongo.Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata kutoka kwa katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa zinasema kuwa viongozi na Wanachama wa CHADEMA walipata taarifa za Jeshi la Polisi kutaka Kutorosha miili ya Marehemu hao ili kuzuia wanachama wa CHADEMA wasiweze kushiriki katika zoezi la Uchunguzi wa miili hiyo (postmortem) na baadala yake wawakilishi wa familia pekee ndio washiriki ambapo ni kinyume na makubaliano ya awali. Viongozi wanaoshikiliwa hadi sasa kwa mujibu wa Dr Slaa ni pamoja na Tundu Lissu, Katibu wa CHADEMA Wa Wilaya ya Tarime na wanachama wengine wa CHADEMA
Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kadri tutakapoendelea kupata taarifa za tukio hilo la Nyamongo Tarime.

No comments: