TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Friday, April 13, 2012

MAMA KANUMBA AZUNGUMZIA HATMA YA LULU

Mama mzazi wa Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtagoa.


MAMA mzazi wa Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtagoa amemzungumzia msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayetuhumiwa kuwa ndiye chanzo cha kifo cha mwanaye na kusema yeye hawezi kumchukia kwani anaamini kilichotokea ni mipango ya Mungu.
Akipiga story na Ijumaa nyumbani kwa marehemu, Vatican Sinza alisema kuwa yeye kwanza hamjui Lulu na wala hajawahi kukutana naye, wala hakuwahi kujua kuwa ana uhusiano na mwanaye kwa sababu hakuwahi kupewa utambulisho.
“Namshukuru Mungu ingawa inauma na ni vigumu kuamini lakini siwezi kumlaumu wala kumchukia mtu, ninachoamini Mungu amempenda zaidi mwanangu na amekufa kama wanavyokufa wengine,” alisema mama huyo kwa masikitiko.

No comments: