TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE
Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com
Friday, March 9, 2012
MADARAKA NA UWAJIBIKAJI: KWA NINI NI VIGUMU SANA KWA VIONGOZI WETU KUJIUZULU???
Ulaya na Marekani uwajibikaji ni jambo la kawaida na linalotegemewa. Kosa au kashfa kidogo tu (hata kama inahusu mambo binafsi) inatosha kumfanya waziri, mbunge, mwakilishi au mshika madaraka ye yote kujiuzulu. Halafu kuna Afrika. Huku kwetu madaraka yanahodhiwa; na ukishayapata basi ni mali yako ya kudumu. Hata uboronge na kufanya madudu namna gani, umo tu. Hata watu walalamike namna gani, umo tu unadunda.…
Ulaya na Marekani uwajibikaji ni jambo la kawaida na linalotegemewa. Kosa au kashfa kidogo tu (hata kama inahusu mambo binafsi) inatosha kumfanya waziri, mbunge, mwakilishi au mshika madaraka ye yote kujiuzulu. Halafu kuna Afrika. Huku kwetu madaraka yanahodhiwa; na ukishayapata basi ni mali yako ya kudumu. Hata uboronge na kufanya madudu namna gani, umo tu. Hata watu walalamike namna gani, umo tu unadunda.
Hebu fikiria kwa mfano huu mgogoro wa madaktari ulioanza, “ukatatuliwa” na sasa umeanza tena. Katika mgomo wa kwanza wagonjwa wengi walipoteza maisha. Ni wazi kwamba hata sasa wagonjwa wengine watapoteza maisha.
Kama dai mojawapo la wagomaji hawa ni kukutaka wewe ujiuzulu, na bila kujali kama una makosa ama la, huwezi kweli kuweka mbele maslahi na maisha ya wagonjwa masikini wasio na kitu na kuwajibika? Ni nini kinachokufanya ufikiri kwamba wewe kubakia madarakani kama Waziri au Katibu Mkuu wa wizara ni muhimu kuliko maisha ya hawa wagonjwa masikini wasio na uwezo wa kwenda kwenye mahospitali ya binafsi au nchi za nje?
Na baada ya kasheshe yote hii, ni kweli bado utasimama mbele ya umma na kujipiga kifua kwamba ungali kiongozi halali na anayejali maisha ya watu unaowaongoza? Una sifa na maarifa gani ya kipekee kiasi kwamba serikali inasimama kidete na kukukingia kifua huku watu wako wakipoteza maisha?
Ni lini viongozi wa Afrika watajifunza kuwajibika na kuanza kuwajali watu wao hasa wale wa tabaka la chini ambao wanawaona kuwa ni wajinga tu na wasio na thamani?
Naamini kwamba siku moja masikini wa Afrika wataamka na kukataa kutendewa kama wanyama. Naamini pia kwamba siku moja Historia itawasamehe viongozi wetu waliowahi kuwajibika na kuachia madaraka kama akina Rostam Aziz, Edward Lowassa na wengineo. Na hawa viongozi vichwamaji wasiowajali watu wao siku moja watajikuta katika shimo la takataka la Historia.
Kwa maoni mbalimbali ya wadau kuhusu mgogoro huu wa serikali na madaktari bofya HAPA.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment