TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Tuesday, February 21, 2012

SUGU NA CLOUDS FM WAPATANISHWA:HILI NI JAMBO LA KUPONGEZWA NA KUDUMISHWA!…


Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakipeana mikono leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Imeelezwa kuwa mkakati huo wa kuwapatanisha ulianza mara baada ya Waziri wa Utamaduni na Michezo, Mhe. Emmanuel Nchimbi, kukutana na Sugu Bungeni wakati wa kikao cha hivi karibuni ambako waziri wakati akiwasilisha muswada wake, alikemea tabia ya kiongozi kuwa na 'visasi', ingawa hakumtaja jina, lakini katika maelezo yake alikuwa akizungumzia 'uadui' uliokuwepo kati ya Ruge na Sugu! HILI NI JAMBO LA KUPONGEZWA NA KUDUMISHWA!


Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliotokana na sababu za kimuziki uliodumu kwa muda wa miaka miwili. Wapatanishi wa mgogoro huo ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu.


No comments: