TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Friday, January 27, 2012

MGOMO WA MADAKTARI, WAGONJWA NAO KUANDAMANA

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda.


KUFUATILIA mgomo wa madaktari nchini, wakidai kuboreshewa masilahi na stahili zao nyingine, sauti za wagonjwa mawodini zimesikika wakisema watalazimika kuandamana endapo hali hiyo itaendelea.
Juzi, Jumatano, Ijumaa lilizunguka katika Hospitali za Mikoa ya Kiafya za Mwananyamala (Kinondoni), Temeke na Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo lilizungumza na wagonjwa walioweka msimamo huo.
AMANA
Kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, mgonjwa mmoja aliyekuwa amelazwa katika wodi ya majeruhi hospitalini hapo, alisema mgomo huo unawaathiri kwa kiasi kikubwa.
“Nipo hapa tangu juzi (Jumatatu), hali yangu ni kama unavyoiona, lakini sijapata matibabu ya uhakika. “Inawezekana wapo sawa kugoma, lakini sisi wagonjwa tunaumia. Kwa nini wasitafute njia nyingine na kumaliza haya mambo?” alisema kwa uchungu mgonjwa huyo.
TEMEKE
Mgonjwa anayesumbuliwa na uvimbe kwenye koo, aliyelazwa katika hospitali hiyo, alisema dawa iliyobaki ni kuandamana ili waweze kupata tiba ya uhakika.
“Afadhali mimi naweza kuzungumza, kuna wengine wana hali mbaya zaidi wapo vitandani. Ndugu mwandishi, madaktari wanakosea na hali ikiendelea hivi tutaandamana,” alisema.
MUHIMBILI
Katika Hospitali ya Muhimbili hali haikuwa nzuri na habari ambazo gazeti hili lilizipata, zinasema kwamba wagonjwa wanaishi kwa hofu kuu.
Felister Emmanuel, anaye muuguza mama yake aliyelazwa katika moja ya wodi zilizopo ndani ya Jengo la Mwaisela alisema: “Madaktari wamegoma, lakini kilichofanyika hapa ni madaktari wastaafu kupewa mikataba ya muda ili waendelee na kazi. Serikali iliangalie hili kwa jicho la tatu.”

No comments: