Chizi alisema Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), tayari imelipatia shirika cheti cha kuruka kiitwacho Air Operators Certificate (AOC) baada ya kuridhishwa jinsi lilivyotekeleza masharti yake.
Hivi karibuni shirika hilo lilizindua mpango wa biashara (Business Plan) ambao unaeleza jinsi lilivyojizatiti kuhakikisha linamudu ushindani wa usafiri wa anga kipindi cha miaka mitano ijayo.
Mpango huo ulizinduliwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Athumani Mfutakamba, ambaye alisifu hatua ya shirika hilo kwa mpango huo endelevu, kupata AOC na kulitakia mafanikio mema.
“Nawapongeza kwa kupata cheti cha kuruka, hii ni fursa kubwa kwa Watanzania kuanza kupata huduma za uhakika za shirika lao, naamini mambo yatakwenda vizuri nawatakia mafanikio mema katika mipango yenu mipya,” alisema Dk Mfutakamba.
TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE
Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com
Tuesday, November 1, 2011
HATIMAYE TWIGA ARUDI ANGANI KWA MBWE MBWE
SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL), leo linatarajia kuanza safari zake mikoa ya Tabora na Kigoma. Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Paul Chizi, alisema ndege hiyo itakuwa ikienda moja kwa moja kwenye mikoa hiyo na safari hizo zitakuwa za kila siku. “Matayarisho yote yamekamilika na ndege tunatarajia itaanza safari zake kama kawaida kuanzia kesho (leo) Novemba Mosi... tunaomba Watanzania watoe ushirikiano kwa shirika lao kwa kuchagua kusafiri na ATCL, maana ni usafiri wa moja kwa moja wa uhakika na salama,” alisema Chizi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment