TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Tuesday, August 23, 2011

SERIKALI YAPELEKA BAJETI MBOVU YA MAJI, HAINA MIKAKATI YA KUWAPUNGUZIA MZIGO WANAWAKE WA KUTAFUTA MAJI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira (kushoto) na Naibu Waziri wa Maji, Gerson Lwenge, wakifuatilia wakati michango ya wabunge walipokuwa wakichangia mjadala wa kupitisha bajeti ya Wizara ya Maji jana.

UPATIKANAJI maji nchini umepanda kutoka
53.7 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 57.8, Desemba 2010.
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira, alisema upatikanaji maji umepanda nchini kutoka asilimia 53.7 mwaka 2005 hadi 57.8 ilipofika Desemba mwaka jana.

Wassira alisoma bajeti hiyo kwa niaba ya Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, ambaye yuko nje ya nchi kwa matibabu.Alisema Serikali kupitia mamlaka za maji safi mijini imeendelea na ujenzi, ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya maji safi kwenye miji mikuu ya mikoa, wilaya na miji midogo.

Kuhusu Dar es Salaam, Wassira alisema upatikanaji maji na miji ya Kibaha na Bagamoyo, zinazohudumiwa na Mamlaka ya Uendeshaji Maji safi na Majitaka (Dawasco), maji yanapatikana kwa asilimia 55 kwa saa tisa kwa siku.

“Kiwango hicho ni kidogo ikilinganishwa na miji mingine, kutokana na kukua kwa Dar es Salaam ikiwa ni ongezeko kubwa la watu ambalo ni asilimia sita kwa mwaka, tofauti na asilimia 4.5 kwenye miji mingine kitaifa,’’ alisema.

Waziri Wassira aliomba Bunge kupitisha Sh446.09 bilioni kwa matumizi ya wizara kipindi cha mwaka 2011/12, ambazo ni fedha za ndani na nje zitakazotumika kwa ajili ya mishahara na matumizi mengine.

Maoni ya upinzani
Hata hivyo, kambi rasmi ya upinzani bungeni iliitaka Serikali kukubali kuwa na mpango wa dharura wa kupeleka umeme Mkoa wa Tabora.

Msemaji wa kambi hiyo, Highness Kiwia, alisema iwapo Serikali haitaweka mpango wa dharura kupeleka umeme, baada ya muda hali itakuwa mbaya kwenye mkoa huo ambao hivi sasa unategemea mpango wa Serikali kupeleka maji kutoka mradi wa Ziwa Victoria.

Kiwia alisema umefika wakati Serikali inatakiwa kufanya dharura kama ilivyofanya kwa Wizara ya Nishati na Madini, ambako iliongeza fedha nyingi kwa ajili ya mradi wa umeme vijijini.

“Mwaka 2014 ni mbali sana, Serikali hii kama ilivyokubali hoja yetu ya kuwa na mpango wa dharura kwenye masuala ya umeme, tunaitaka sasa ije na mpango wa dharura kuhakikisha mji huo unapata maji mapema iwezekanavyo,’’ alisema Kiwia.

Kiwia, ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela, alisema ili Tanzania iweze kufanikiwa kuwa na uhakika wa maji kwenye majiji na miji, lazima kuwapo na mamlaka za maji ambazo ni imara na zenye kufanya kazi kwa kiwango.

Alisema tatizo kubwa linalosumbua mamlaka nyingi nchini, ni mitandao mibovu ambayo imechakaa na haijabadilishwa kwa muda mrefu.Tatizo lingine ni wizi wa maji na matumizi mabaya ya fedha kwenye miradi hususan ile ya vijijini.

No comments: