TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA NA UONE FAIDA YAKE

Kwa Habari au Tangazo lolote la Biashara tuwasiliane kwa Simu 0713 - 581741 au 0755 - 863097.Email: robadio8@gmail.com

Thursday, July 19, 2012

TAARIFA YA IKULU KUHUSU AJALI YA MV SKAGIT


JANA tarehe 18 Julai, 2012, majira ya alasiri kumetokea ajali ya kuzama kwa meli ya MV SKAGIT katika eneo la Chumbe, Zanzibar.  Meli hiyo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kueleka Zanzibar ilikuwa imebeba watu 290. Kati yao watu wazima 250, watoto 31 na wafanyakazi wa meli 9.
Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliagiza vyombo vya ulinzi na usalama vya Serikali ya Muungano yaani JWTZ na  Polisi waanze kazi ya uokoaji mara moja.
          Kazi hiyo imefanywa kwa kushirikiana na vyombo vya usalama vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na meli za makampuni binafsi.  Mpaka giza lilipokuwa limeingia na hivyo kazi ya uokoaji kusitishwa mpaka kutakapokucha tarehe 19 Julai, 2012, watu 136 walikuwa wameokolewa na maiti 31 zilikuwa zimepatikana.  Aidha, mali zilizokuwa kwenye meli hiyo hazikuweza kuokolewa.
          Kufuatia ajali hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano alizungumza na Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.  Alimpa pole kwa ajali iliyotokea hasa kwa vifo na majeraha waliyopata Watanzania wenzetu na watu wasiokuwa raia wa Tanzania.  Alimuomba afikishe salamu za rambirambi kwa ndugu zetu waliopotelewa na jamaa zao na kuwapa pole waliopata majeraha na maumivu maungoni mwao. Rais wa Jamhuri ya Muungano alisema kuwa huu ni msiba wetu sote na kwamba majonzi yao ni majonzi yake na ya Watanzania wote.  Kwa ndugu zetu waliojeruhiwa tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape ahueni na wapone haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao za kujiletea maendeleo na kulijenga taifa letu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wote wa ngazi mbalimbali kwa uongozi wao thabiti tangu taarifa ya kutokea kwa ajali mpaka sasa.  Aidha, amewapongeza maafisa na askari wa vyombo vya ulinzi na usalama na wafanyakazi wa meli binafsi, kwa juhudi kubwa walizozifanya za uokoaji wa ndugu zetu waliopatwa na maafa haya makubwa na ya aina yake.  Amewataka waendeleze juhudi hizo leo na siku zijazo.
          Rais amewataka wananchi wawe na moyo wa subira na uvumilivu wakati kazi ya uokoaji inaendelea.  Kama ilivyofanyika katika ajali ya MV Spice Islander miezi 10 iliyopita, uchunguzi wa kina utafanyika kubaini chanzo cha ajali.
          Kutokana na ajali hiyo na msiba huu mkubwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ametangaza maombolezo ya taifa ya siku tatu ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia leo, tarehe 19 Julai, 2012.
          Asanteni sana.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.

Tuesday, July 10, 2012

CHAMA CHA MADAKTARI CHAWASILISHA MAOMBI UN YA ULINZI KWA VIONGOZI WAKE


Monday, July 9, 2012

VIONGOZI WA DINI WANTAKA KIKWETE KUKUTANA NA MADAKTARI TENA

 "Viongozi wa dini wakiomba dua ya pamoja na Madaktari na baadhi ya wanaharakati kutoka katika mashirika tofauti.Wa kwanza kulia ni kaka Badi Darusi mmoja wa wanaharakati aliekuwepo katika mkutano huo.

VIONGOZI wa dini za Kikristo na Kiislamu wamejitosa katika sakata la Dk Steven Ulimboka ambaye yuko nchini Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kutekwa na kupigwa na watu wasiojulikana pamoja na mgomo wa madaktari kwa kufanya mkutano na viongozi wa Jumuiya ya madaktari na wanaharakati jijini Dar es Salaam jana.
Viongozi hao walipendekeza iundwe kamati huru ya kuchunguza tukio la kupigwa Dk Ulimboka mapema iwezekanavyo ili kupata ukweli wa kilichotokea.
Pia viongozi hao walishauri kuwa Rais Kikwete akutane na madaktari pamoja na viongozi wa dini ili kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wao unaoendelea nchini hivi sasa.Viongozi hao pia wameitaka Serikali kutoa ulinzi kwa Dk Ulimboka na madaktari wote wengine ili kuwahakikishia usalama wa maisha yao.
Akisoma tamko la viongozi hao, Mkurugenzi wa Baraza la Habari la Kiislamu(Bahakita), Hussein Msopa kwa niaba ya viongozi hao alisema kwamba, kuundwa kwa kamati huru ya uchunguzi  itasaidia kupata ukweli wa tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dk Ulimboka na kuwezesha  kubaini wahusika wa tukio hilo.
“Tukio la kutekwa, kuteswa na kutupwa katika Msitu wa Pande Dk Ulimboka ni la kusikitisha… na tunamuomba Rais Kikwete aunde tume huru itakayojumuisha madaktari wenyewe, viongozi wa dini, wanaharakati na wanasheria kubaini kiini cha tatizo hilo.” alisema Msopa.
Kauli ya viongozi hao wa dini ni ya kwanza kutolewa kwa pamoja tangu kutokea kwa tukio la kutekwa, kupigwa na kutupwa kwa Dk Ulimboka katika Msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Viongozi hao pamoja na kudai tume huru pia waliomba Serikali kufuta kesi  iliyofungua dhidi ya madaktari waliofukuzwa kutokana na mgomo na  kuwarejesha kazini ili  kumaliza mgomo huo waliodai unaathiri afya za Watanzania.
Tamko hilo limekuja siku chache tangu Serikali  ilipofungua kesi dhidi ya madaktari waliogoma kwa Baraza la Madaktari Tanzania ikilitaka kufanya uchunguzi na kuchukua hatua stahiki kwa madaktari hao.
Msopa alitaja sababu ya viongozi hao kuungana na wanaharakati kutafuta suluhisho la mgomo huo kuwa ni kuona Watanzania wanazidi kuteseka kwa kukosa huduma za matibabu.
“Tunafahamu kwamba, Rais Kikwete ameweza kutatua migogoro mingi mfano mgogoro wa Chadema, suala la Katiba Mpya, migogoro ya Zanzibar, hivyo pia sasa tunaamini katika hili la madaktari ataweza kulitafutia ufumbuzi,” alisema Msopa.
Kwa upande wake Mchungaji Lawrance Mzava wa Kanisa la Kiinjili la Assemblies of God (EAGT) Ubungo ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, alisema hiyo itakuwa njia sahihi ya kumaliza mgogoro huo unaotikisa nchi kwa sasa.
“Njia sahihi ya kuondoa mgogoro huo ni kufanya mazungumzo ambayo yatasaidia kufikia makubaliano yatakayoleta  ufumbuzi wa kudumu  wa mgomo wa madaktari,” alisema Mzava na kuongeza:
“Sisi  tunaamini kuwa njia sahihi ya kuleta  suluhu ya mgogoro huu ni kwa Rais  Kikwete kukutana na  kufanya  mazungumzo na sisi (viongozi wa dini) na madaktari,” alisema.
Mgomo
Mgomo wa madaktari unaoelezwa kumalizika kwa kusuasua ulianza Juni 23 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI) na kusambaa hospitali mbalimbali nchini, madaktari wakitoa madai mbalimbali kuitaka Serikali iyatekeleze.

Hata hivyo, hadi jana upatikanaji wa huduma MNH  na Taasisi ya Mifupa (MOI), umezidi kuzorota, huku baadhi ya madaktari wakisema tukio la Dk Ulimboka limewapunguzia ari ya kufanya kazi.

Wakizungumza  kwa sharti la kutotajwa majina, baadhi ya madaktari wa MNH, walisema tukio la kutekwa, kupigwa na kutupwa kwa Dk Ulimboka  limewatisha.

“Kwa sasa madaktari hawana ari, hata wakifika eneo la kazi bado suala la kufanya kazi ni kitu kingine, lakini kitendo cha kutekwa kwa Dk Ulimboka kimetutisha sana, ” alisema mmoja wa madaktari hao wa MNH.

Uchunguzi wa Blog hii  umebaini kuwapo kwa baadhi ya madaktari bingwa katika MNH pamoja na MOI, ambao nao walithibitisha kuwa utendaji kazi hauwezi kuwa wa ufanisi kwa njia ya kulazimishwa.

“Serikali inachotakiwa siyo kulazimisha, inapaswa kusikiliza na kutatua hoja, sisi madai yetu yamepotoshwa, hatuna vifaa vya kufanyia kazi, lakini wananchi hilo hawalielewi,” alisema mmoja wa madaktari hao.

Hata hivyo, Msemaji wa MNH, Eminael Aligaesha alisisitiza kuwa huduma katika hospitali hiyo zinarejea hatua kwa hatua.

Thursday, June 28, 2012

A PUBLIC STATEMENT ON THE CRUEL, INHUMAN AND DEGRADING ATTACT TO A HUMAN RIGHT DEFENDER- DR.ULIMBOKA

                                                                           PRESS RELEASE

The Legal and Human Rights Centre (LHRC) jointly with The Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRD- Coalition)) seriously condemn the barbaric and savage attack that was directed to Dr. Steven Ulimboka the chairperson of Tanzania Doctors Association on 26TH June, 2012 at around mid night in Dar es Salaam.
Wherefore, we would like to inform the general public that, unknown group of individuals [most likely alleged to be state agents] on the said date and time, at Leader’s Club Area, in Kinondoni District, in Dar es Salaam City, arrested the said Dr. Ulimboka. They forced him into a car [one black saloon car] - which did not have plate numbers; they took him away by force and held him; they covered his face with a piece of black cloth and tied him with ropes, while beating him severely using different objects such as gun-butts [butt-stocks], and other sharp-edged weapons. As a result of those savage beatings, he sustained several visible injuries in different parts of his body from head to feet. In short he was kidnapped and brutally tortured.
At the dawn of 27th June, we were informed of the event and that the said Dr. Ulimboka, who was earlier on reported missing, was found and that was held at Bunju Police Station. We were informed Dr. Ulimboka was found unconscious by good Samaritans in a forest at Mabwepande in Dar es Salaam where he was lying without assistance after being that much hurt and bleeding excessively. The residents took him to a nearby police Station at Bunju. We intervened at Bunju police post and picked him for treatment where he is currently being diagnosed at the Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI) for medical examination and treatment.
Given this cruel, inhumane and degrading incidence, LHRC and THRD-Coalition and on behalf of the rest of likeminded organisations and individual human rights defenders, with all our energy and vigour, seriously and gravely condemn this intolerable and callous attack to Dr. Ulimboka.
We call upon,
a) The Government of the United Republic of Tanzania,
i. To provide all medical services as the case may be, so as to salvage the life of Dr. Ulimboka;
ii. To objectively and thoroughly investigate the whole incidence;
1
iii. To apprehend all perpetrators and their agents and publicly notify the nation about them and the reasons for inflicting such terrible injuries to the said Dr. Ulimboka;
iv. To professionally prosecute all perpetrators;
v. To ensure that the perpetrators are adequately penalized upon conviction.
b)The Police Force:
- To abstain from taking sides in the existing labour dispute between the doctors and the government;
- To respect rule of law, human rights, presumption of innocence and professionalism in all of their undertakings.
c) The Human Rights Defenders:
- To form and consolidate our Solidarity at all levels and condemn the attack and the like.
d) The Medical Professionals:
- Considering the presence of a provocative environment that invites negative reaction, we still call upon all medical professionals to refrain from active confrontation at this moment and proceed to pursue their rights within the ambit of the law.
e) The general Public,
- To support all initiatives that are meant to pursue ends of justice in relation to this incident.
- To demand accountability and improvement of social services in particular – health services in Tanzania.
- To condemn such incidences of abuse of human rights.
Wherefore, all what was done to Dr. Ulimboka are carrying series of criminal liabilities to perpetrators. Moreover, the incidence demonstrates a clear violation of his basic rights as protected by the United Republic of Tanzania Constitution of 1977 articles 12, 13, 14, 15,16,17 18, 20, 22, 23 and 29.
WE believe that such incidences like this one are normally calculated to silence and hamper the work and efforts of human rights defenders. It should never be repeated in our civilized and democratic society otherwise all human rights defenders in Tanzania are at peril.
Delivered in Dar es Salaam Tanzania, this 2 7th June 2012.
Executive Director – LHRC Coordinator – THRD-Coalition
Dr. Helen Kijo-Bisimba Mr. Onesmo Olengurumwa
2

Thursday, May 17, 2012

KAULI YA BAVICHA KUHUSIANA NA KAULI ILIYOTOLEWA NA JOHN SHIBUDA


Mbunge wa Maswa Magharibi (CHADEMA) John Shibuda akisalimiana na Rais Kikwete.
 
BAVICHA imepokea kwa mshituko mkubwa kauli ya ndugu Shibuda kuwa yeye atagombea Urais na Meneja wake wa Kampeni atakuwa Mwenyekiti wa CCM ndugu Jakaya Kikwete, na alitoa kauli hiyo kwenye kikao cha NEC ya CCM.
MAMBO YAFUATAYO YEMETUSHTUA;
1.    Katoa Kauli hiyo kwenye kikao cha NEC ya CCM 
2.    Meneja wa kampeni zake amemtangaza kuwa ni Mwenyekiti wa CCM taifa Jakaya Kikwete
3.    Amesema kuwa hakuna chama kingine chenye uwezo wa kuiongoza nchi kwa sasa.
4.    Alitoa tamko hilo kwa niaba ya APRM .
Mambo hayo manne ndio yametushtua na kutufedhehesha sana sisi vijana wa CHADEMA na ndio maana tumelazimika kutoa kauli kuhusiana na suala hili , na kauli yetu ni kama ifuatavyo;
1. Kamwe BAVICHA hatutaruhusu mgombea Urais wa CHADEMA meneja wake wa kampeni awe ni Mwenyekiti wa CCM hata siku moja kwani tunao watu wa kutosha na wenye uwezo wa kutosha kuifanya kazi hiyo na hatuhitaji msaada huo .
2.    Kamwe hatutaruhusu mgombea urais wa CHADEMA awe anatangaza nia kwenye vikiao vya CCM kwani hawana mamlaka ya kumteua mgombea wa CHADEMA na kama Shibuda alikuwa halijui hilo anapaswa kulifahamu kuanzia sasa kuwa vijana wa CHADEMA hatuchaguliwi mgombea na NEC ya CCM kwani CHADEMA kuna vikao na taratibu zetu za kuteua wagombea.
3.    Kusema kuwa hakuna chama kingine chenye uwezo wa kuongoza nchi ni kutudhalilisha sisi vijana wa CHADEMA na watanzania wote ambao leo wanaiona CHADEMA kama tumaini pekee la kuwakomboa, kauli hii tunaamini kama vijana wa CHADEMA kuwa mamlaka za nidhamu hazitakaa kimya na kuiachia kauli ya namna hii iachwe bila kutakiwa maelezo ya kina , tutaitisha kikao cha BARAZA na tutaijadili kauli hii na kuwasilisha mapendekezo yetu kwenye vikao halali vya chama .
4.    Tunapenda kumwambia kuwa kama anaona kuwa yeye haendani na utamaduni wa chama chetu na anakiona kuwa hakina uwezo  wa kuongoza dola anafanya nini kwenye chama ambacho anona kuwa hakiwezi kuongoza dola? Kwanini atafute urais kwenye chama ambacho anaona hakiwezi kuongoza dola ? anawatania watanzania? Ni heri akaenda kwenye hicho ambacho anaamini kuwa kinaweza kuongoza dola , kwani lengo la chama chochote kile ni kuchukua dola na sio vinginevyo.
5.    Mwisho tunapenda kuwahakikishia vijana wote wa Tanzania na wananchi kwa ujumla kuwa tayari CHADEMA kimejiandaa kikamilifu kuongoza dola na wasiwe na hofu na maneno yaliyotamkwa na Mbunge huyu .
6.    Natoa wito kwa Vijana wenzangu wote wa CHADEMA kuwa sasa tujiandae kikamilifu katika kukabiliana na mtu yeyote yule ambaye ataonekana kuwa kikwazo kwa chama chetu na wananchi kwa ujumla wake katika kuelekea kuchukua dola 2015 .
Nawatakia kila la kheri katika ujenzi wa chama na tuendeleze operesheni ya ‘Vua Gamba, Vaa Gwanda’ popote pale tulipo nchini.
        Imetolewa leo Dar es Salaam,
 Mei 16, 2012 na;
John Heche
Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa.

Tuesday, May 15, 2012

NJEMBA AFUMWA AKIMCHUNA MBWA!

 


 Bwana Rajabu akimchuna mbwa kama alivyokutwa na kamera yetu.



Hapa akipakia Mzoga wake mara baada ya Kuuchuna





Rajabu akiwa kafungwa mikono baada ya kula kichapo.   




Habari kwa hisani ya Global Publishers